Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

KAVUMBAGU AIDHARAU SAFU YA ULINZI YA SIMBA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Didier Kavumbagu, raia wa Burundi, ameitazama vizuri safu ya ulinzi ya timu ya Simba akajigamba kuwa bado ni 'cha mtoto' dhidi ya safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Kavumbagu, ambaye alisajiliwa na Yanga msimu uliopita akitokea Olympique ya Burundi, alisema kuwa hana presha kabisa na ukuta wa Simba, unaoongozwa na Kaze Gilbert, ambaye anamfahamu vizuri tangu kwao nchini Burundi, walikowahi kucheza wote soka.

Alisema anaufahamu vizuri uwezo wa Kaze, kwani hawezi kucheza mipira ya purukushani.
Alisema kwamba mbali na kumfahamu Kaze, bado hajaona uimara wa ukuta huo, huku akisisitiza kuwa siku timu hizo zitakapokutana ni lazima Yanga iibuke na ushindi wa mabao mengi.

"Ninamheshimu sana Kaze, ila katika timu ya Simba sitamuangalia beki huyo pekee, bali ninachokiangalia zaidi ni ukuta wa timu hiyo, nikiamini kuwa Kaze anahitaji muda kuzoea mpira wa Tanzania ambao ni wa nguvu zaidi," alisema.

Kavumbagu alisema kwamba kutokana na Ligi ya Tanzania kuwa ya kutumia nguvu zaidi, ana imani kuwa hawezi kushindwa kupenya kwenye ukuta huo mwepesi.

Simba imekuwa na tatizo katika safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu mabao karibu kila mechi, tatizo ambalo kocha wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni analikiri.

No comments:

Post a Comment