Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, September 8, 2013

BALE AVAMIWA NA MASHABIKI UWANJANI NA KINDA SCHALKE AELEZA KILICHOMFANYA AZITOSE ARSENAL, CHELSEA NA MAN CITY




SKOPJE, Macedonia

MCHEZAJI ghali duniani, Gareth Bale, amejikuta kwenye wakati mgumu, baada ya kuvamiwa na mashabiki wawili uwanjani.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, mshambuliaji huyo ambaye Real Madrid imemsajili msimu huu kwa kitita cha pauni milioni 86, alikumbana na mkasa huo wakati akiwa na timu yake ya taifa ya Wales, akipasha misuli  timu zikiwa mapumziko katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Macedonia.

Gazeti hilo lilieleza wakati mshambuliaji huyo wa pembeni wa timu ya Taifa ya Wales akipasha misuli na mchezaji mwenzake  wa akiba, Adam Matthews,  ghafla mashabiki wawili wakaingia uwanjani na kuanza kumzonga nyota huyo.

Lilieleza, kutokana na hali hiyo, ilibidi kiungo wa Celtic, Matthews  kuingilia kati ili kumnusuru Bale kabla ya maofisa usalama hawajaingilia kati kuwadhibiti vijana hao na huku  Bale akionekana kupuuzia tukio hilo baada ya kuonekana akicheka.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa inambidi nyota huyo mwenye umri wa miaka  24 kuchukua tahadhari kutokana na umaarufu aliojiwekea tangu ajiunge na Real Madrid, akitokea Tottenham kwa kile kinachodaiwa huenda akawa akiandamwa na mashabiki.

Katika mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia jana mjini Skopje, Bale alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba kutokana na hali ya wasiwasi kuhusu afya yake na hakuonekana uwanjani hata baada ya timu yake kufungwa mabao 2-1.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 
Kinda Schalke aeleza kilichomfanya azitose Arsenal, Chelsea na Manchester City
SCHALKE, Ujerumani

NYOTA wa timu ya Schalke ya nchini Ujerumani, Julian Draxler, amefunguka akisema kuwa aliamua kuzitosa timu kongwe za Ligi Kuu ya England kutokana na kutamani  kukipiga kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Draxler alisema jana kuwa mwanzoni mwa majira haya ya joto alikuwa na mawazo ya kwenda kukipiga nje ya nchi hiyo, lakini kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 akasema kuwa baadaye alighairi na kuamua kuendelea kuitumikia klabu yake ya Schalke.
Hata hivyo, nyota huyo anasema kuwa pamoja na kubadili mawazo, milango bado ipo wazi endapo ofa zitajitokeza siku za mbele.
Kabla ya kubadili mawazo yake, inaelezwa kuwa  timu za Arsenal, Chelsea na Manchester City zilikuwa zikipigana vikumbo zikimwania nyota huyo.

No comments:

Post a Comment