Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, September 8, 2013

SIRI YA ARSENAL KUMNASA OZIL HANDARANI




LONDON, England
SIRI ya timu ya Arsenal kumnasa kiungo wa timu ya Real Madrid, Mesut Ozil, imebainika, baada ya kuelezwa  kwamba Manchester United walichelewa kutuma ofa  kwa ajili ya kumnasa nyota mwingine wa timu hiyo, Sami Khedira.

Gazeti la  El Economista  lilieleza jana kuwa Real Madrid  ilikuwa na mpango wa kumuuza Khedira  badala ya Ozil, kutokana na kuwa  ilikuwa ni lazima iuze mchezaji mmojawapo kwa ajili ya kukamilisha usajili wa  Gareth Bale.

Gazeti hilo lilieleza kuwa hata hivyo ofa ya Manchester United ya pauni milioni 34 iliyokuwa ikimtaka Khedira iliwasilishwa mjini Madrid ikiwa imechelewa, lakini ikapokelewa wakati  mkataba wa Arsenal kwa  Mesut Ozil ulikuwa ukijadiliwa kwa muda wa  wiki kadhaa na baada ya kufikia makubaliano ya awali  baina ya klabu hizo mbili, Rais wa Real Madrid,  Florentino Perez akakubali.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa klabu hiyo ya Old Trafford iliwasilisha ombi lake la kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 saa moja kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hali ambayo ilisababisha ombi hilo lisifanikiwe.

"Kwa ujumla hatukuwa na muda wa kulijadili jambo hilo,” alisema Ozil.
"Nilikuwa na mazungumzo na kocha mpya, Carlo Ancelotti  wiki chache zilizopita na ilikuwa ikionekana wazi kwangu mimi nitabaki  Real Madrid,” aliongeza.
Alisema kuwa wao kama wachezaji huwa hawana ushawishi kusajiliwa kwa bei mbaya  na kwamba Real Madrid ndiyo waliokataa ofa ya Manchester United  na akasema kuwa hata hivyo anafurahi kwa hilo.

No comments:

Post a Comment