Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 23, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAHIDI MAKUBWA WACHEZAJI WA TAIFA STARS WAKATI WA CHAKULA CHA MCHANA LEO


Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo  mingine  ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya  kushiriki  mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014. Picha na 2 
Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo  mingine  ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya  kushiriki  mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014. Picha na 4 
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars mara baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7 ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia. Picha na 5 
Meneja wa Timu ya Taifa Stars Bw. Mukebesi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya Taifa Stars Juma Kaseja Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete. Picha no 3 
Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars wakipata chakula walichoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo alipokutana nao kuwatakia ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco. Picha na 6 
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Picha na 7 
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam.

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuwafanyia makubwa wachezaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' iwapo watashinda katika michezo yao ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Stars inajiwinda na mchezo dhidi ya Morocco utakaofanyika Juni 8 mwaka huu nchini Morocco.

Rais Kikwete alisema timu hiyo imetoka mbali na sasa imepiga hatua kubwa na matunda yake yanaoneka hivyo hatakuwa nyuma kuhakikisha wachezaji wake wanapata kitu cha kumbukumbu.

Kikwete alisema kama timu hiyo itaendelea kufanya vizuri na kuongoza katika kundi lake ataifanyia timu hiyo chochote itakachohitaji na kitu hicho kitakuwa kumbukumbu hata wakistaafu kuichezea timu hiyo.

Alisema kitu kikubwa ambacho wachezaji wanatakiwa kufanya kwa sasa ni kuhakikisha mawazo yao na akili zao wanazielekeza katika michezo yao na si kitu kingine.

"Sasa hivi elekezeni nguvu zenu katika michezo yenu na mhakikishe mnashinda mambo mengine niachieni mimi pamoja na Kamati ya Saidia Stars Ishinde," alisema Rais Kikwete.

Alisema timu imeonyesha matumaini kwa kufanya vizuri katika michezo yake lakini kitu kikubwa anachotaka ni kuhakikisha inashinda katika mchezo wa Morocco na kuongoza kundi lake.

Alisema kuanzia sasa wasikubali kushindwa ili waweze kupata nafasi na hata kama Ivory Coast itakuja kucheza nyumbani wahakikishe wanaifunga kwani uwezo walionao wao ndio walionao wachezaji wa Tanzania.

"Mechi zilizobaki ni ngumu lakini najua mkijiamini na kujijenga kisaikolojia michezo hiyo si migumu na sitakuwa nyuma kuwatakia heri ili mshinde," alisema.

Stars inashika nafasi ya pili katika kundi C ikiwa na pointi sita nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba ambapo timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia na Morocco.

Pia wachezaji nao wameahidi kucheza kwa jihad wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho na kuiwezesha timu yao kushinda katika mchezo wa marudiano dhidi ya Morocco.

Stars itajitupa dimbani Juni 8 mwaka huu kucheza mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Kapteni wa timu hiyo, Juma Kaseja, alisema hayo Ikulu Dar es Salaam jana,  katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Rais Kikwete.

Kaseja alisema timu yake itahakikisha inafanikisha hilo baada ya serikali na Rais Jakaya Kikwete kutoa sapoti kubwa kwa timu hiyo kila inapokuwa na mashindano.

Kaseja alisema serikali ya awamu ya nne imeipa kipaumbele kikubwa timu hiyo na huku rais akitoa hamasa za mara kwa mara kwa timu hiyo.

Alisema kutokana na hali hiyo, timu yake haina sababu ya kushindwa kumtoa kimasomaso rais kwa kupamba katika michezo yake.

"Naishukuru serikali pamoja na Rais Kikwete kwa kuwa nasi bega kwa bega na ni jambo la faraja kuona rais pamoja na serikali yake ipo nasi kwa kila hatua," alisema Kaseja.

Alisema anaahidi ushindi kwa timu yake na atahakikisha anaiongoza vyema timu yake ili iweze kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment