Breaking News!!!!! NIYONZIMA ASAINI YANGA MKATABA WA MIAKA MIWILI
Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili na kuendelea kubaki Yanga.
Akizungumza na Salehjembe, Niyomzima amesema amefanikiwa kusaini Yanga mkataba huo.
“Kweli nilifuatwa na timu nyingi sana na zilinipa ofa kubwa, moja ya timu ni kutoka Tunisia.
“Nyingine ni za hapa Tanzania, lakini nilikuwa nina mipango yangu na nimeamua kusaini,” alisema Niyonzima raia wa Rwanda.
Kuna taarifa Yanga itamtambulisha Niyonzima leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo.
Kwa hisani ya Salehjembe blog
Post a Comment