Wednesday, May 15, 2013
KAMBI YA VIJANA YA BAISKELI KWA NCHI ZA AFRIKA KUFANYIKA BABATI TANZANIA
NCHI saba zinatarajia kushiriki kambi ya vipaji vya mchezo wa baiskeli Afrika inayotarajia kuanza Mei 24 hadi Juni 2 Wilayani Babati jijini Arusha.
Akizungumza na Lenzi ya Michezo , Katibu Mkuu wa Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA), Lado Haule alisema Tanzania itashirikisha wachezaji tisa na makocha watatu.
Haule alizitaja nchi zilizothibitisha kushiriki kambi hiyo ni pamoja na Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la mchezo huo la Kimataifa (UCI), Malawi, Kenya, Uganda, Rwanda, Namibia na Ethiopia.
Aidha Haule alisema Tanzania itawakilishwa na makocha watatu waliofaulu kozi ya Kimataifa ya mchezo iliyofanyika jijini Arusha mwaka 2010 ambao ni Nassoro Haji, Lucas Bupilipili na Godfrey Mhagama ‘Jax’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment