Ukiwa sasa umepita mwezi mmoja na nusu toka kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu Dar es salaam, mwigizaji Kajala ameahidi kuigiza movie moja ambayo itahusisha maisha yake kuanzia kesi yake ilipoanza mpaka yeye kuingia gerezani na kutoka.
Kajala ambae March 25, 2013 aliachiwa huru na Mahakama baada ya mwigizaji Wema Sepetu kumlipia faini ya shilingi za Kitanzania milioni 13 na kukwepa kifungo cha miaka mitano jela, amesema movie ya maisha yake atakayocheza itatosheleza kwenye part 1 na part 2.
Kwa sasa Kajala anacheza movie nyingine akiwa chini ya kampuni ya mwigizaji Wema Sepetu lakini amesema tayari stori kuhusu movie ya maisha yake jela imeshaanza kufanyiwa kazi japo bado mume wake yupo gerezani wakati huu.
Kabla ya Kajala kuachiwa huru, ni makosa matatu yalikua yakiwakabili yeye na mume wake, ambapo kosa la kwanza ni kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala Dar es salaam.
Kosa la pili ni kwamba April 14, 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34 na sheria ya kupambana na rushwa ya mwaka 2007, na shitaka la tatu ni kutakatisha fedha ambalo walilitenda April 14, 2010 Pamoja na kwamba mwigizaji Kajala yuko chini ya kampuni ya mwigizaji Wema Sepetu, wawili hawa pia ni marafiki wakubwa ambapo wema uliofanywa na Wema Sepetu kumlipia faini ya milioni 13 umemfanya Kajala kuamua kuchora tattoo mwilini mwake yenye jina la Wema huku akisisitiza kwamba hana kingine cha kumlipa.
Kajala amesema gerezani alikuta Wanawake ambao idadi yake inafika kwenye 160 mpaka 170 ambapo Wanawake wengi wamemwambia kilichowapeleka jela ni kesi za mauaji ya watoto wachanga wanaozaliwa.
No comments:
Post a Comment