KIUNGO
wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kwamba sasa ameweka kando mambo yote na
kusisitiza kuwa moyo wake, mwili na akili vyote vinatamani kuona anaifunga Simba
katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaofanyika Jumamosi hii.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Rwanda, Niyonzima maarufu kama Fabregas, ambaye kwa sasa
anaripotiwa kuwindwa kwa udi na uvumba na Simba, alisema hajali lolote kwenye
hilo zaidi ya kuwafunga mahasimu wao hao wakati timu yake itakapomenyana nao
katika mchezo wa funga dimba la Ligi Kuu Bara msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam Jumamosi hii.
Niyonzima,
ambaye anaaminika kuwa kiungo bora kabisa kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara,
aliliambia DIMBA ameweka pembeni masuala yote ya kuhusu hatima yake ya msimu
ujao zaidi ya kuitumikia klabu yake ya sasa na kuhakikisha anaipatia ushindi
ili kuweka heshima dhidi ya mahasimu wao.
"Kwa
sasa akili yangu ipo kwenye mechi hii. Moyo na fikira zangu zote zipo kwenye
kuifunga Simba na kuipa heshima Yanga," alisema.
Kuhusu
ubora wa mkali huyo wa Amavubi, Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Mwina Kaduguda,
alisema ametazama nyota wote wanaocheza soka hapa nchini na kusisitiza kwamba
kiungo huyo ndiye anayestahili kuendelea kubaki hapa nchini miongoni mwa nyota
wote wa kimataifa.
Kaduguda
alisema ni wazi kabisa mchezaji huyo anastahili kulipwa mshahara mkubwa,
kutokana na kazi yake isiyokuwa na shaka anayofanya ndani ya uwanja na kwamba
Yanga inapaswa kushukuru kwa kuwa na mchezaji huyo kwenye kikosi chao.
Kiungo
wa zamani wa Simba, Selemani Matola, amekikubali kiwango cha Niyonzima na
kuwataka Simba kama wana mpango wa kumnasa mchezaji huyo basi watimize jambo
hilo kwani ni mchezaji mwenye kila kigezo cha kuwachezea miamba hao wa
Msimbazi.
Matola
alisema uongozi wa klabu hiyo ya Simba unapaswa kutazama mahitaji ya benchi la
ufundi na kama kutakuwa na ombi la kusajiliwa kwa mchezaji kama Niyonzima, basi
wasilipuuzie hilo na walifanye kwa nguvu zote, kwasababu litakuwa na faida
kubwa kwa klabu hiyo.
Alisema
Niyonzima ni mchezaji mzuri ataweza kusaidia Simba msimu ujao endapo
watafanikiwa kumnasa ila ana uhakika kiungo huyo kutoka kwa kipindi kirefu
katika klabu hiyo, kwasababu dhamira yake ni kwenda kucheza soka ng'ambo.
“Endapo
Simba watafanikiwa kumchukua na kumsajili atakuwa msaada mkubwa katika kikosi
hicho cha msimu ujao, ambapo uongozi huo umeonyesha nia ya kutaka kufanya
usajili ili kufanya kweli katika ligi msimu ujao,” alisema Matola.
Niyonzima
kwa sasa analitikisa soko la usajili wa soka la Tanzania, baada ya kuwindwa na
klabu kadha, Simba na Azam FC huku klabu yake ya Yanga ikidai kwamba
imemsainisha mkataba wa miaka miwili mchezaji huyo kitu ambacho kiungo mwenyewe
amekikana na kufanya mchakato wa kuwania saini yake kupamba moto.
No comments:
Post a Comment