TIMU ya Elimu Fc juzi imetwaa Ubingwa wa mashindano ya Esther Bulaya Cup
kwa Mwaka 2013 baada ya kuifunga Bunda Sport Club kwa penalti 3-1 baada ya
mchezo kumalizika kwa kufungana 1-1.
Elimu FC ilijinyakulia kombe pamoja na shilingi milioni moja na mshindi
wa pili alipata 500,000 na mshindi wa
tatu Town Stars waliokuwa mabingwa watetezi walipata 300,000 pamoja na seti
moja jezi.
Mashindano haya yanadhaminiwa na Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Vijana
(CCM) Esther Bulaya, na yalizikutanisha timu 30 za wilaya ya Bunda mkoa wa
Mara.
Akiongea kwa
simu na BINGWA, Ester Bulaya ambaye ni Mbunge wa viti maalum kupitia Vijana
(CCM) alisema anashukuru mashindano
yamemalizika na bingwa kupatikana ila kulikuwepo na baadhi ya watu ambao
walipanga mikakati ya kuhujumu yasifanyike.
“Kuna baadhi
ya watu walitaka kuhujuma ila wajue kuwa kufanya hivyo siyo kwamba wananikomoa
mimi bali watakuwa hawawatendei haki Vijana wa Bunda ambao ndiyo walengwa katika
kukuza vipaji vyao”, alisema Ester.
Pia alisema
vijana ambao walionyesha viwango vizuri katika soka watatafutiwa timu pia ataendela kudhamini mashindano hayo yachezwe katika wilaya zote
za mkoa wa Mara kwani yeye ni Mbunge wa vija wote bila kujali itikadi za vyama
Michuano hiyo ya Esther Bulaya Cup 2013 iliunganisha Michezo mbalimbali ikiwemo
Michezo ya bao,draft pamoja na Pool table,ambapo na kila mchezo zawadi mbambali
zilitolewa na kughalimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 12 kwa mwaka huu.
|
|
No comments:
Post a Comment