Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, May 5, 2013

CRISTIANO RONALDO AIONGOZA REAL MADRID KUIFUNGA REAL VALLADOLID BAO 4-1.


Real Madid jana iliichapa Real Valladolid Bao 4-3 huku Cristiano Ronaldo akifunga Bao 2 na kufanya idadi yake ya Magoli kufikia 199 chini ya Misimu minne hapo Madrid ikiwa ni Rekodi kwa Klabu hiyo. 

Bao nyingine za Real zilifungwa na Kaka na Valiente aliejifunga mwenyewe.

Cristiano Ronaldo alifunga bao 2 na kufikisha mabao 199 akikaribia kuvunja rekodi hapo Madrid
Ronaldo akiruka juu kupiga mpira kwa kichwa zaidi ya kipa wa Real Valladolid
Lakini Mechi hii itakumbukwa sana kwa matukio ya baada ya Mechi pale Mourinho alipomsifia Kipa wake Diego Lopez kwa kudai anatamani angemsaini Kipa huyo mapema mno kuliko kumchukua Januari Mwaka huu.
Lopez amekuwa ndie Kipa Nambari Wani wa Real na kumfanya Kipa wa Timu ya Taifa ya Spain, Iker Casillas, awe hana namba.

Lakini kauli hiyo ya Mourinho ilijibiwa vikali na Mchezaji wa Real, Pepe, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Ureno, ambae alitamka: “Kuna haja ya kumwonyshea heshima kidogo Casillas. Anapendwa hapa. Alichosema Kocha hakistahili. Casillas ni sehemu ya Madrid. Yeye ni Nguli kwa Klabu na Spain.” 


Huku kukiwa na minong’ono kuwa Mourinho ataihama Real mwishoni mwa Msimu akitarajiwa kwenda Chelsea, Kocha Msaidizi wa Real, Aitor Karanka, alijaribu kuuzima mgongano huo kwa kusema: “Sijasikia alichosema Pepe na kama alisema hivyo ukweli ni kuwa katika Miaka mitatu ya kufanya kazi hapa hakuna Mtu ambae haheshimiwi na kutomuheshimu Mchezaji mmoja ni kuvunjia heshima Wachezaji wote 25. Siku zote tumechagua Wachezaji 11 ambao tunatarajia watashinda. Hatuchukui Mtu kwa muonekano wake. Kuvunja heshima ni pale kutomteua Mchezaji anaecheza vizuri na kumchukua mwingine. Hatuvunji heshima hapa.”
WAFUNGAJI WANAOONGOZA KWA KUZIONA NYAVU ZAIDI.
44 Lionel Messi (Barcelona) 33 Cristiano Ronaldo (Real Madrid) 26 Radamel Falcao (Atletico Madrid) 19 Alvaro Negredo (Sevilla) Roberto Soldado (Valencia) 16 Ruben Castro (Real Betis) 15 Piti (Rayo Vallecano)

No comments:

Post a Comment