Serikali mbioni kuanzisha Wakala wa kusimamia miundombinu ya michezo nchini



Serikali imetangaza kuwa mchakato wa kuunda chombo maalumu kitakachokuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza miundombinu ya michezo nchini umefika hatua za mwisho.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalumu), Profesa Palamagamba Kabudi, wakati wa hafla ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri, akiwemo kikosi cha Taifa Stars kilichotinga hatua ya 16 bora katika michuano ya AFCON 2025.

Profesa Kabudi alifafanua kuwa wakala huyo atakuwa na jukumu la kuhakikisha viwanja vya mpira wa miguu, maeneo ya michezo mingine, na kumbi za burudani nchini kote yanabaki katika hali bora wakati wote. 

Alisema wamejifunza kutoka katika gharama kubwa iliyotumika kukarabati uwanja wa Benjamin Mkapa  kwani umejengwa hapakuwepo na usimamizi wa mkuangalia ukarfabati wa aina yoyote ile.

“Taratibu za kuanzisha wakalawa serikali kusimamia miundombinu ya michezo nchini umefika kwenye hatua nzuri,” alisema Profesa

Kabudi. 

Miundombinu hiyo ni pamoja na viwanja vya mpira wa miguu, michezo mingine na burudani.

Tanzania itakayokuwa mwenyeji wa Afcon 2027 sambamba na Kenya na Uganda, inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya michuano hiyo.


No comments