Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 1, 2013

BAYERN MUNICH YAIFUNGA BARCELONA NYUMBANI KWAO 3-0 UEFA CHAMPIONS LEAGUE, YAIONDOA KWA MABAO 7-0, FAINALI SASA KUZIKUTANISHA TIMU ZA UJERUMANI TU

Huko Nou Camp Mashabiki wakidhani Barcelona watapindua kipigo cha awali cha 4-0 walichopewa na Bayern Munich kwenye Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LEAGUE, lakini leo Bayern Munich wameendeleza kipondo kwa kuibonda tena Barca Bao 3-0 na wao kutinga Fainali watakayocheza na wenzao Borussia Dortmund. 

Hii ni Fainali ya 3 kwa Bayern Munich, ambao wako chini ya Kocha Jupp Heynckes ambae mwishoni mwa Msimu anaondoka na Msimu ujao kuja Kocha wa zamani wa Barca Pep Guardiola, kutinga ndani ya Miaka minne
Mwaka jana walitolewa na Chelsea kwa Mikwaju ya Penati tano tano kwenye Fainali iliyochezwa huko Allianz Arena Mjini Munich ambako ndio Uwanja wa Nyumbani wa Bayern Munich.
Lionel Messi hakucheza, alibaki Benchi, na bila ya yeye, baadhi ya Wadau hunena ni sawa na QPR na leo ndani ya Uwanja wao Nou Camp hilo limedhihirika kwa kuwafuata wenzao Real Madrid ambao jana walibwagwa nje na Borussia Dortmund.Mchezaji Xavi Hernandez wa Barcelona akiachia shuti kali ambalo limepita juu ya postiMchezaji mtata na mgumu Arjen Robben wa Munich akiwapatia bao la kwanza Bayern leo hii usiku huko Nou Camp

Wakijiuliza kipi kilichowasibu... Gerard Pique, David Villa na Cesc Fabregas ili wakitibu haraka

Marc Bartra akianguka chini na aliyesimama ni mchezaji Mario Mandzukic
Arjen Robben akipongezana na wachezaji wenzie hapa baada ya kuona wanazidi kusonga mbeleKocha wa Bayern Jupp Heyncke akishangilia baada Arjen Robben kufungua bao la kwanza na kuwaweka katika nafasi nzuri ya kuelekea fainaliGerard Pique akijifunga dakika ya 72 na kufanya  2-0 na kuwapa Bayern bao la kuongoza zaidiGerard Pique anavyoonekana baada ya kujipigilia ukutani kwa msumari wa moto na kuwapa bao BayernThomas Mullerakawawasha bao jingine la tatu dakika ya 76 nakufanya bao kuwa 3-0

London calling: Bayern Munich goalkeeper Manuel Neuer (left) and his team-mates have a final date
Kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer (kushoto)kwa furaha zao kuelekea Fainali itakayofanyika tarehe
25 Mei 2013 UWANJA wa WEMBLEY, London.
Wachezaji wa Bayern kwa raha zao baada ya mechi usiku huu.
VIKOSI:
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra (Montoya 87), Adriano, Xavi (Sanchez 55), Song, Iniesta (Thiago 64), Villa, Fabregas, Pedro.
Subs not used: Pinto, Messi, Jonathan, Montoya, Tello.
Booked: Dani Alves
Bayern Munich: Neuer, Lahm (Rafinha 77), Boateng, Van Buyten, Alaba, Javi Martinez (Tymoschuk 74), Schweinsteiger, (Gustavo 66) Robben, Muller, Ribery, Mandzukic.
Subs not used: Starke, Dante, Shaqiri,Gomez.
Goals: Robben 49, Pique o.g. 72, Muller 76
Booked: Robben
Referee: Damir Skomina (Slovenia)

No comments:

Post a Comment