DORTMUND, Ujerumani
LICHA ya umakini alionao katika suala zima la utikisaji nyavu kama alivyothibitisha juzi usiku, Roberto Lewandowski hakuwa gumzo sana kuelekea mechi dhidi ya Real Madrid kwenye dimba la Signal Iduna Park yaliko makazi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Gumzo kuelekea mechi hiyo iliyoisha kwa wenyeji kushinda mabao 4-1, Lewandowski akifunga yote upande wa Dortmund, Gotze alikuwa gumzo, huku mashabiki wa klabu hiyo wakitishia kususia kuingia dimbani hapo kutokana na tamko la klabu hiyo kuwa imemuuza mkali huyo kwa Bayern Munich.
Kutokana na tishio hilo la mashabiki, uongozi wa Dortmund uliwaomba mashabiki wafike kwa wingi na kwamba walilazimika kukubali ofa ya Bayern baada ya Gotze kuonesha kuhitaji kutoka na kwamba hakuna kitakachoharibika licha ya kuondoka kwake.
Mashabiki wakapunguza jazba zao kwa uongozi na kuamua kuingia uwanjani kama kawaida, lakini wakahamishia hasira zao mapema hata kabla ya filimbi ya kuanza mechi hiyo, kwa kuonesha mabango ya 'kumponda' Gotze, huku wakimuita Msaliti Yuda kutokana na kuhamia Allianz Arena.
Zomeazomea juu yake, uchomaji moto jezi yake na mabango tofauti yakionesha walivyokasirishwa na uamuzi wake, 'vikamtoa' mchezoni nyota huyo, ingawa hiyo haikumzuiwa Lewandowski kufanya mambo makubwa akitumia sapoti ya nyota wengine na mchango mdogo wa Gotze.
Zifuatazo ni picha tofauti kumuhusu Gotze aliyeuzwa kwa pauni milioni 32 kwa mabingwa wapya wa Bundesliga, Bayern Munich maarufu kama The Bavarian.
Gotze (kulia), akichuana na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo katiika mecgi ya nusu fainali mabingwa Ulaya iliyoisha kwa Dortmund kuiadabisha Madrid kwa mabao 4-1.
Mashabiki wakionesha tambara kubwa lililoandikwa Gotze Raus 'Ondoka Gotze' kama ishara ya kukerwa na uamuzi wake wa kuihama klabu hiyo.
Gotze akiwa katika moja ya mechi za Dortmund.
Jezi ya zamani ya ugenini ya Borussia Dortmund inayovaliwa na Mario Gotze, ikichomwa moto kabla ya kuanza kwa mechi dhidi ya Madrid.
Moto ukishika kasi kuunguza jezi ya Gotze.
Judas 'Yuda', nadhani ndilo jina ambalo mashabiki waliona anastahili kuitwa Gotze kama jezi yake ionavyooneshwa hapo na mashabiki hao.
Hata hivyo, wapo waliotambua uhuru alionao Gotze katika kuamua juu ya hatia yake klabuni kwao, ndio maana wenginme hawakusita kumshukurukwa mchango aliotoa wakati wote wa kuichezea Dortmund. Pichani bango lililoandika DANKE MARIO yaani AHSANTE MARIO.
No comments:
Post a Comment