Waimbaji wa Mlimani Park 'Sikinde' Hassani Kunyata, Abdallah Hemba na Hassani Bitchuka
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde'
inatarajiwa kutambulisha nyimbo zake mpya katika miji kadhaa wakati wakielekea
Mbeya katika sherehe za Mei Mosi.
Sikinde imealikwa kutumbuiza katika sherehe hizo ambazo kitaifa zitafanyikia
kwenye mkoa huo wa Mbeya wiki ijayo.
Akizungumza na BINGWA, Katibu wa bendi hiyo, Hamis Milambo alisema wakiwa njiani kuelekea Mbeya watafanya
maonyesho kadhaa katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Mbeya na nje mkoahuo.
Milambo alisema maonyesho hayo yataanza kesho Ijumaa watakapotambulisha
nyimbo zao kwenye ukumbi wa Comfort Chamazi na jumamosi wakuwa City Pub uliopo
Mwanjelwa.
Siku ya jumapili watatumbuiza Tunduma kabla ya siku ya Mei
Mosi kutumbuiza kwenye sherehe za Mei mosi asubuhi kwenye Uwanja wa Sokoine na
usiku watakuwa na shoo kubwa kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa Mbeya.
"Siku ya Mei Mosi tukishatumbuiza Uwanja wa Sokoine tutafanya onyesho
katika ukumbi maarufu wa Benjamin Mkapa
na kuanza kuanza safari ya kurejea Dar kuendelea na mengine," alisema
Milambo.
Milambo anasema katika maonyesho yote watatambulisha nyimbo zao wanazoziandaa
kwa ajili ya albamu mpya ya ambazo ni 'Jinamizi la Talaka', 'Kuvunjika kwa Dole
Gumba', 'Nundule' na nyingine pia tutawapa burudani ya nyimbo za zilizoifanya
Sikinde kutambuliwa kama mabingwa wa Muziki wa Dansi Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment