Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 22, 2013

KIPA WA ARSENALSCSZESNY AIOMBA RADHI KUTOKANA NA MANENO YA BABA YAKE JUU YA WENGER


KIPA wa Arsenal, Wojciech Szczesny, ameomba radhi kwa kauli ya Baba yake kumshambulia Meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger.
Jana Baba yake Mzazi Kipa huyo, Maciej Szczesny, ambae alikuwa Mchezaji wa Kimataifa wa Poland, alimtaka Arsène Wenger awajibike kwa kuporomoka kiwango kwa Kipa wake Wojciech Szczesny badala ya kumgeuza ‘Mbuzi wa Kafara’.

Lakini leo, Wojciech Szczesny, akiwa kwenye Timu ya Taifa ya Poland akigombea namba na Kipa mwenzake Artur Boruc wa Southampton kwa ajili ya Mechi za Kombe la Dunia, ametoa maelezo kupitia Tovuti ya Arsenal ambako ameomba radhi na kusema yale yalikuwa ni maneno ya Baba yake na si yake.
Kipa huyo amedai maneno ya Baba yake yamevunja heshima kwa Klabu anayoipenda na amesisitiza kuwa Siku zote, kwa Miaka 7 aliyokuwa Klabuni hapo, ameonyesha heshima kwa Klabu, Wenger, Makocha wote, Wachezaji wenzake na Mashabiki.

Ametamka: “Siku zote nimepata sapoti kubwa toka kwa Meneja na Mashabiki na sasa natilia mkazo kurudi hali yangu bora. Nasikia fahari kuwa sehemu ya Arsenal na natarajia kuwa hapa muda mrefu!”Szczesny akimpongeza Lukasz Fabianski kwa kazi nzuri baada ya kuifunga 2-0 Swansea jumamosi iliyopita.

No comments:

Post a Comment