JUMA NKAMIA AMPA SOMO RAGE KUHUSU MGOGORO WA SIMBA
Aliwahi kuwa katibu
mwenezi wa klabu ya Simba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kondoa kusini Juma
Selemani Nkamia amesema kujiuzulu kwa viongozi wa klabu ya Simba ni pigo kwa
klabu hiyo na kwamba kuna haja ya mwenyekiti wa klabu hiyo kutafakari juu ya
mustakabali wa klabu hiyo haraka iwezekanavyo.Amesema Has Poppe amekuwa na mchangano mkubwa katika klabu ya Simba tangu wakati ule akiwa ni kiongozi wa klabu hiyo na kwamba huenda kuna tatizo kubwa ambalo kiongozi huyo ameliona na kuona bora akae pembeni jambo ambalo linatahitaji tafakari ya kina ya wanachama.
Nkamia amesema huenda tatizo likawa ni kwa mwenyekiti wa klabu hiyo kupingana na maamuzi ya vikao halali vya wajumbe wa kamati ya utendaji au kujiamulia mambo yake mwenyewe hali ambayo huenda ikapelekea wajumbe wengine wakafuata nyayo hizo na kuleta athari kubwa kwa klabu hasa wakati huu ligi ikiwa inaelekea ukingoni.
Amemuomba mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaji Ismail Aden Rage kufanya busara kwa kulitazama jambo hili kwa makini sana kwani huenda yeye akawa ndiyo tatizo ndani ya klabu hiyo.
Post a Comment