RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Leodegar Tenga amemshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenela Mukangara kwa kukubali ombi la Shirikisho la kutaka kukutana
naye kwa mazungumzo na kumsihi asitishe hatua anazodhamiria kuchukua hadi hapo
kikao hicho kitakapofanyika.
Waziri Mukangara ameiagiza TFF kuitisha
Mkutano Mkuu wa marekebisho ya katiba ifikapo tarehe 15 Aprili 2013 na Mkutano
Mkuu wa Uchaguzi ifikapo tarehe 25 Mei 2013 na kwamba tamko la TFF kutekeleza
maagizo hayo liwe limetolewa katika muda wa siku tano zinazoishia Jumatatu
(Machi 11, 2013).
Katika barua
pepe ambayo amemuandikia Waziri ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi, Rais Tenga
ameeleza kuwa alikwenda ofisini kwake tarehe 7 Machi 2013 kujaribu kumuona
lakini akaambiwa amesafiri, hivyo kuomba kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara,
ambaye pia hakuwepo ofisini na hatimaye akakutana na Naibu Katibu
Mkuu.
Katika barua
hiyo pepe, Rais Tenga ameeleza madhumuni ya kutaka kuonana na Waziri Mukangara
kuwa ni kwanza “kukushukuru kwa kukubali kuonana na ujumbe wa TFF ulioongozwa na
mjumbe wetu wa Kamati ya Utendaji, Bw. Alex Mgongolwa, akiongozana na Katibu
Mkuu wa TFF, Bw. Angetile Osiah, jana tarehe 6 Machi
2013.
“Kukushukuru
kwa kukubali kukutana nasi tena siku ya tarehe 19 Machi, kwa ajili ya mazungumzo
juu ya maagizo yako.
“Kukuarifu
kuwa nimepokea maagizo yako uliyoyatoa jana kupitia kwa Mjumbe wetu wa Kamati ya
Utendaji na kwa njia ya barua; na
“Kwa heshima na taadhima, kukuomba usitishe hatua yoyote ile unayodhamiria kuchukua hadi hapo tutakapokutana na kupata maelezo yetu, TFF, juu ya maamuzi na maagizo uliyoyatoa.”
“Kwa heshima na taadhima, kukuomba usitishe hatua yoyote ile unayodhamiria kuchukua hadi hapo tutakapokutana na kupata maelezo yetu, TFF, juu ya maamuzi na maagizo uliyoyatoa.”
Tenga,
ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika
(CAF) aliondoka jana (Machi 7 mwaka huu) kwenda Marrakech, Morocco kuhudhuria
kikao cha kamati hiyo na pia Mkutano Mkuu wa CAF ambao umepangwa kufanyika Machi
10 mwaka huu ukihusisha pia ajenda ya uchaguzi wa rais.
No comments:
Post a Comment