Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 23, 2013

ENGLAND YAFANYA MAUAJI, YAIFUMUA SAN MARINO 8-0 KUTAFUTA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014


Leo England wakicheza mchezo wa kuwania kusafiri kwenda Brazil Mwaka 2014 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia na San Marino wameibwagiza mabao 8 kwa , Bao la kwanza wameanza kwa kujifunga kupitia mchezaji wao Alessandro Della Valle dakika ya 12. Mchezaji wa Arsenal Oxlade-Chamberlain akaipatia England bao dakika ya 28, mchezaji wa Spurs Defoe akaongeza bao la 3 dakika ya 36 na dakika ya 77 kipindi cha pili, Mchezaji wa Manchester United Young akawapatia bao jingine 39 kabla ya Lampard kufunga bao dakika ya 42 kabla ya mapumziko, kipindi cha pili pamoja na wachezaji wa San Marino kucheza vizuri kuziba nafasi zilizokuwa zinapwaya mchezaji matata wa United Wayne Rooney amewafunga bao dakika ya 54, na mchezaji wa Chelsea Sturridge akawapachikia bao la 8 dakika ya 70.


Wachezaji wa England wakifurahia baada ya kupata bao la kwanza

Alex Oxlade-Chamberlain akitupia bao la pili baada ya bao la kwanza la kujifunga
Jermain Defoe akitupia bao la tatu usiku huu.

Jermain Defoe akimzungusha kipa kiaina na kummaliza kimya kimya

Ashley Young akifunga bao la mbali 35 yards 
Frank Lampard naye hakufanya makosa akatupia hapa

Wayne Rooney akiifungia bao timu yake dakika ya 54 kipindi cha pili
Daniel Sturridge akiimaliza goli la mwisho
VIKOSI:
San Marino: Aldo Simoncini, Fabio Vitaioli, Palazzi, Alessandro Della Valle, Davide Simoncini, Cervellini, Gasperoni, Cibelli (Buscarini 68), Fabio Bollini, Selva (Rinaldi 75), Matteo Vitaioli.
Subs: Federico Valentini, Bacciocchi, Bianchi, Coppini, Alex Della Valle, Carlo Valentini, Vannucci.
England: Hart, Walker, Smalling, Lescott, Baines, Oxlade-Chamberlain, Lampard (Parker 67), Cleverley (Osman 56), Young, Rooney (Sturridge 56), Defoe.

Subs: Foster, Cole, Taylor, Caulker, Milner, Gerrard, Carrick, Welbeck, Forster.
Goal: Alessandro Della Valle (og) 12, Oxlade-Chamberlain 28, Defoe 36, 77, Young 39, Lampard 42, Rooney 54, Sturridge 70.
Referee: Alain Bieri (Switzerland)

No comments:

Post a Comment