Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 22, 2013

CHINUA ACHEBE AFARIKI DUNIA


Chinua Achebe, mwandishi wa vitabu vya fasihi
Mwandishi Maarufu wa vitabu duniani Chinua Achebe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika kwa ujumla.
Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua Achebe kuwa mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika kipindi chake, ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa wale wote waliomfahamu.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha kwanza cha fasihi kitwaacho'Things Fall Apart', ambacho alikitunga mwaka 1958 kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.
Kitabu hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake katika jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za mgaharibi na kijadi.

Alipata ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani mwaka 1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi ya mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa katika ajali ya gari.
Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.


Wasifu wa Chinua Achebe 
Mtunga riwaya na mtu mashuhuri wa taifa la Nigeria , Chinua Achebe, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, Bilkisu Labaran anaelezea wasifu wa mwandishi huyo 

Chinua Achebe anasikfika kuwa ni baba wa fasihi ya Afrika. Kila mtoto wa shule barani Afrika atakuwa amesoma kitabu chake mashuhuri kabisa Things Fall Apart. Kimefasiriwa kwa lugha kadhaa ikiwemo ya Kiswahili. Hamkani si shwari tena. Ni hadithi ya Okonkwo-mkulima ambae anapambana kuhifadhi mila na utamaduni wake licha ya shinikizo kutoka wakoloni Waingereza.

Achebe amewahamasisha watunzi wa barani Afrika na duniani kote na tungo zake zimesifiwa kwa kujivunia utamaduni wake wa Kiigbo kusini Mashariki mwa Nigeria.
Uzalendo wake wa Mwaafrika ulimfanya atupilie mbali jina lake la kwanza la Kiingereza-Albert-na badala yake kujiita Chinua.

Alizaliwa mnamo mwaka 1930, na kuanza kutunga riwaya katika miaka ya mwisho ya 1950 katika mkesha wa vuguvugu la kupigania uhuru barani Afrika. Na sifa hasa za Chinua Achebe's zinatokana na jinsi tungo zake zilivyosaidia mwamko wa mageuzi ya kimapinduzi katika Afrika.

Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Nigeria katika miaka ya 60 aliunga mkono Jamhuri iliyojitenga ya Biafra .Baada ya vita Achebe alijitosa katika kampeni za kutetea demokrasia na utawala bora..

Lakini baada ya Nigeria kukumbwa na mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi na machafuko, alielezea ghadhabu zake kuhusu jinsi nchi ilivyotawaliwa na kubainisha msimamo wake alikataa tunzo zote za taifa alizotunukiwa na serikali.

No comments:

Post a Comment