Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 24, 2013

TAIFA STARS YAWAPA RAHA WATANZANIA YAITANDIKA MOROCCO 3-1 TAIFA

TIMU ya Taifa "Taifa Stars"  leo imeiibwaga Morocco mabao 3-1 katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.

Washambuliaji wawili wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu waliofunga mabao hayo.
Samatta alifunga mawili na Ulimwengu aliyetokea benchi dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto alifunga moja.

Kwa matokeo hayo, Stars inaendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi C kwa pointi sita, nyuma ya Ivory Coast inayoongoza kwa pointi saba, baada ya jana kushinda 3-0 dhidi ya Gambia.

Kipindi cha pili, Stars walianza na mabadiliko, kocha Kim Poulsen akimtoa Kazimoto na kumuingiza Ulimwengu aliyekwenda kubadilisha  mchezo.
Katika dakika ya 46, mpira wa kwanza kuugusa Thomas Ulimwengu ambao alirushiwa na beki Erasto Nyoni aliunganisha nyavuni na kuipatia Stars bao la kwanza.

Bao hilo liliongeza kasi ya mchezo kwa upande wa Stars na katika dakika ya 67, Samatta alifunga bao la pili akimchambua kipa Nadir Lamyaghri baada ya kupokea pasi ya Ulimwengu na kuifanya Morocco kuchanganyikiwa baada ya bao la pili na kuruhusu Stars kutawala zaidi mchezo.

Kama vile siyo Stars walikuwa wanapiga pasi zisizo na idadi na kuwapa burudani mashabiki wa soka wa Tanzania waliyokuwa waliokuwa wamejaa uwanja bila kujali mvua iliyonyesha mchana na kusababisha mafuriko sehemu kadhaa za jiji la Da r es Salaam
Kazi nzuri ya Ulimwengu aliyepambana na beki wa Morocco na kumzidi nguvu hatimaye kufanikiwa kupiga krosi, iliyoipatia Stars bao la tatu lililozamishwa kimiani na Samatta dakika ya 80.

Beki Abderrahim Achchakir alipewa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya Stars kufunga bao la tatu. Beki huyo alikuwa kama analalamika kuchezewa rafu na Ulimwengu wakati akipiga krosi ya bao.
Baada ya bao la tatu wachezaji wa Stars walionyesha burudani kwa kugongeana pasi nyingi hata hivyo kosa kidogo la safu ya ulinzi liliipa nafasi Morocco kupata bao lililofungwa na Yousef Elarabi aliyetokea benchi. 

Baada ya mchezo huo, kocha wa Tanzania, Kim Poulsen alisema kwamba amefurahia matokeo na anawapongeza vijana, lakini bado ana kazi ngumu katika mechi tatu zijazo dhidi ya Morocco na Gambia ugenini na Ivory Coast nyumbani. 

Naye kocha wa Morocco, Rachid Taoussi pamoja na kujutia nafasi nyingi walizopoteza, alisema matokeo hayo yamemsikitisha kwani yanawaweka katika wakati mgumu kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Hata hivyo, alisema yamechangiwa na kuwa na timu mpya ya wachezaji chipukizi, lakini watajipanga zaidi kwa mechi zilizobaki wafanye vizuri na kufufua matumaini.

Katika mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk 63, Frank Domayo, Mbwana Samatta/John Bocco dk 91, Mwinyi Kazimoto/Thomas Ulimwengu dk46 na Amri Kiemba.

Morocco; Nadir Lamyaghri, Younes Belakhadr, Abdelilah Hafidi/Nuredenne Amrabat, Zakarya Bergdich, Abderrahim Achchakir, Younes Hammal, Abdelaziz Barrada, Issam Eladoua, Kamal Chafni, Chahir Belghazouani/Youssef El Arabi na Hamza Abourazouk.  



No comments:

Post a Comment