Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 25, 2013

RUVU SHOOTING INAIENDELA COASTAL UNION KWA TAHADHARI, YAWASILISHA VIELELEZO VYA FUJO ZA MSIMU ULIOPITA TFF

UONGOZI wa timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani umewasilisha kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Nchini (TFF), Boniface Wambura DVD ya video inayoonesha vurugu zilizotokea katika mchezo namba 127 dhidi ya Coastal Union msimu uliopita uliochezwa Februari 19 2012 katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Baada ya mchezo huo Ruvu Shooting walilalamikia uamuzi mbovu kutoka kwa mwamuzi iliyechezesha mechi hiyo na hivyo kutokea vurugu waliyofanyiwa kutoka kwa wachezaji na mashabiki wa timu ya Coastal.

Akizungumza jana, Ofisa Habari wa timu ya Ruvu, Masau Bwire, alisema kuwa mwamuzi wa mchezo huo aliwaonea na kuwapendelea wenyeji hao na baada ya mpira kumalizika wachezaji pamoja na mashabiki wa Coastal walivamia wachezaji wa Ruvu pamoja na benchi zima la ufundi na kuanza kuwashambulia.

Bwire alisema kuwa aliyekuwa msimamizi wa kitua hicho cha Tanga, Makamu Mwenyekiti wa Mashindano hayo Walis Kalia aliitisha mkutano na waandishi wa Habari na kukanusha kauli iliyotolewa na yeye juu ya timu hiyo kufanyiwa vurugu.

"Aliyekuwa Mwenyekiti na Msimamizi wa kituo kile, aliitisha mkutano na waandishi wa Habari na kudai kuwa Ofosa Habari wa Ruvu aliongea uongo na kuwa hawakufanyiwa vurugu hizo ndani wala nje ya Uwanja huo," alisema Bwire.

Alisema kuwa uongozi wa TFF ulikubaliana na kauli hiyo ya Kalia na kuushutumu uongozi wa Ruvu Shooting kwa kusema uongo kupitia msemaji wake Masau Bwire aliyetoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.

"Kwa kuonesha kuwa tulikuwa sahihi na kauli yetu ya kufanyiwa vuguru hizo, tumeamua kupeleka DVD hiyo yenye picha za sehemu ya mchezo huo ili TFF ione hali halisi ya mchezo huo hususani vurugu zilizojitokeza," alisema Bwire.

Aliongeza kuwa kesho timu yake inashuka dimbani  katika Uwanja huo huo kucheza na Coastal wameamua kuchukua tahadhali kutokana na kuwa na mazoea ya kuwafanyia vurugu kila wanapokutana katika Uwanja huo.

akizungumzia mchezo wao wa kesho Bwire alisema kuwa wamejiandaa vilivyo na matumaini yao ni kuibuka na ushindi katika mechi hiyo ili kuwaonesha Coastal kuwa uwezo wao kisoka ni mdogo ukilinganisha na Ruvu Shooting.






No comments:

Post a Comment