YANGA YAINGIA KAMBINI TANSOMA KUJIWINDA NA KAGERA SUGAR
VINARA wa Ligi Kuu Yanga SC, wameingia kambini leo katika Hotel ya Tansoma kujiandaa na mechi yao ya jumatano dhidi ya Kagera Sugar mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Akizungumza leo, Ofisa Habari wa klabu hiyo Baraka Kiziguto alisema kuwa, timu hiyo imeingia kambini kutokana na mapendekezo ya Kocha Mkuu Ernie Brandts.
Kiziguto alisema timu hiyo ikiwa kambini inaendelea na mazoezi ya katika Uwanja wa Bora Kijitonyama, na baada ya mechi hiyo watasikiliza tena maamuzi ya Kocha kama kuendelea na kambi hiyo au la.
"Timu imeingia kambini kutokana na mapendekezo ya Kocha kujiandaa na mechi ya keshokutwa (kesho), na baada ya hapo Kocha ataamua kuendelea kukaa hapo au la," alisema Kiziguto.
Aliongeza kuwa Kocha alitoa maamuzi hayo kutokana na kuwa Ligi Ngumu kwa sasa kwani kila timu inajiandaa kufa na kupona katika hatua za kuelekea mwishoni.
Yanga ipo katika nafasi ya kwanza ya Ligi hiyo ikiwa na pointi 39, inatarajia kushuka dimbani kesho katika mechi yake dhidi ya Kagera Sugar.
No comments:
Post a Comment