Mechi namba
121 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 24 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Mtibwa Sugar kuibuka ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Simba imeingiza sh.
239,686,000.
Watazamaji
10,669 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
14,577,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
9,467,694.92.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia
watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 9,491 na kuingiza sh.
47,455,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000
kilichovutia washabiki 105 na kuingiza sh.
2,100,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15
ya uwanja sh. 7,412,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh.
4,447,297.36, Kamati ya Ligi sh. 4,447,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 2,223,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,729,504.53.
No comments:
Post a Comment