Mwamuzi msaidizi Fredinand Chacha (wa kwanza kushoto) akitoka uwanjani baada ya mchezo wa Simba na Mtibwa. Wengine ni Ibrahim Kidiwa na Samwel Mpenzu |
Mwamuzi
Msaidizi wa FIFA, Ferdinand Chacha ameondolewa kuchezesha mechi za VPL baada ya
kupata alama za chini kwenye mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa
mwezi uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waamuzi wanaopata alama 6.5 au
chini ya hapo kati ya 10 zinazohitajika pia wanaondolewa kwenye mechi za VPL na
FDL.
Waamuzi
wengine walioondolewa kwa kutomudu mechi walizochezesha za VPL ni Mathew Akrama
(Yanga vs Simba), Ephrony Ndissa (Yanga vs Simba), Ronald Swai (Yanga vs Mtibwa
Sugar).
Walioondolewa kwa kupata alama za chini ni
Alex Mahagi (Simba vs JKT Ruvu), Methusela Musebula (Toto Africans vs Coastal
Union), Lingstone Lwiza (Toto Africans vs Coastal Union), Idd Mikongoti (Toto
Africans vs Mtibwa Sugar) na Samson Kobe (Toto Africans vs Mtibwa
Sugar).
Masoud Mkelemi aliyekuwa mwamuzi wa mezani
katika mechi ya FDL kati ya Moro United na Villa Squad ameondolewa kwa kutofika
kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na alichelewa kwa
dakika tano kufika uwanjani
Wakati huo huo Baadhi ya makamishna wa VPL na FDL wameondolewa
na wengine kusimamishwa kusimamia mechi za ligi hizo kutokana na upungufu kwenye
ripoti zao au kutowasilisha kabisa ripoti hizo TFF baada ya
mechi.
Kamishna
Mohamed Jumbe aliyesimamia mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba ameondolewa
kwenye orodha ya makamishna kutokana na ripoti yake kuwa na
upungufu.
Makamishna
wa mechi kati ya JKT Oljoro vs Yanga (Hakim Byemba), JKT Oljoro vs Kagera Sugar
(Salum Kikwamba), Toto Africans vs African Lyon (Charles Komba), Coastal Union
vs JKT Oljoro (Mohamed Nyange) wamesimamishwa hadi watakapowasilisha ripoti zao
TFF.
Kwa upande wa FDL makamishna waliosimamishwa
hadi watakapowasilisha ripoti zao TFF ni wa mechi kati ya Kurugenzi vs Polisi
Iringa, Morani vs Mwadui, Polisi Mara vs Pamba, Polisi Mara vs Mwadui, Morani vs
JKT Kanembwa na Pamba vs Polisi Dodoma.
Wengine ni Mwadui vs JKT Kanembwa, Polisi
Tabora vs Morani, Polisi Dodoma vs Polisi Mara, Polisi Tabora vs Mwadui, Polisi
Mara vs Morani, JKT Kanembwa vs Polisi Mara, Morani vs Rhino Rangers na Small
Kids vs Mkamba Rangers.
Kamati ya Ligi imewakumbusha makamishna wote
kuwa ni jukumu lao kuhakikisha ripoti zao zimefika TFF na kurekebisha upungufu
wa jinsi ya kuripoti matukio yanayotokea uwanjani. Licha ya kutuma nakala kwa
njia ya email, wanatakiwa pia kuwasilisha ripoti halisi (original)
TFF.
No comments:
Post a Comment