TIMU KUONGEZWA KOMBE LA DUNIA LA KLABU
SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) linatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia la Klabu baada ya kuanza mchakato wa kupanua mashindano hayo kutoka timu 32 hadi 48 kuanzia mwaka 2029.Hatua hiyo inakuja baada ya FIFA kufikia makubaliano ya kuunda ubia mpya na kundi la Klabu za Ulaya (EFC), linalowakilisha zaidi ya klabu 700 barani humo na linaloongozwa na Rais wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, ushirikiano huo unatarajiwa kufungua milango kwa klabu nyingi zaidi kutoka Ligi Kuu England kushiriki mashindano hayo, jambo ambalo litakuwa pigo kwa timu zilizokuwa zikikosa nafasi kutokana na kanuni zilizokuwapo awali.
Katika toleo la kwanza la mashindano yaliyopanuliwa na kushirikisha timu 32, baadhi ya mabingwa wa ligi kubwa za Ulaya walishindwa kushiriki kutokana na FIFA kuweka kikomo cha timu mbili kutoka kila nchi pamoja na kuzingatia washindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na viwango vya ubora vya UEFA.

Post a Comment