Michael Richard Wambura akionyesha katiba ambayo matumizi yake yamesitishwa na Waziri wakati akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni |
Sekretarieti
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya Serikali
ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella
Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini
kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la
2012.
Baada ya kupokea barua hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu), Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kujadili tamko hilo.
Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya TFF kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment