Wachezaji hao ni washambuliaji John Bocco, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya DR Congo, ambao ni wagonjwa.
Akizungumza leo Daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa alisema
Bocco hataweza kucheza kutokana na kuumia goti katika michuano ya Kombe la
Chalenji iliyomalizika Desemba 8, mwaka huu Kampala Uganda.
Mwankemwa alisema, pamoja na kukosa mchezo huo, ataendelea kuwepo kambini
kwani aliumia akiwa kwenye timu hiyo.
Akifafanua kuhusu Samatta na Ulimwengu, alisema wao waliumia wakiwa na timu
yao ya TP Mazembe na wamekuja na vyeti vinavyoonyesha kuwa wagonjwa.
Mwankemwa alisema, cheti cha Ulimwengu kinaonyesha aliumia goti la mguu wa
kulia na Samatta yeye kinaonyesha aliumia bega.
Wachezaji hao ambao waliwasili nchini na kuendelea kukaa nyumbani, juzi
walipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyiwa kipimo cha MRI ili wapate
tiba sahihi.
Alisema wanasubiri vipimo vya daktari kutoka Muhimbili ila kweli wachezaji
hao ni majeruhi na wataendelea kuwatibu ili waweze kupona.
"Tunawatibu ili tutakapoingia kambini Januari 6, mwakani kujiandaa
na mashindano ya Fainali za Mataifa ya
Afrika (AFCON), wawe wamepona kabisa', alisema Mwankemwa.
Wapinzani
wa Stars walitua leo jioni nchini kwa ajili ya mchezo huo, ambao utachezwa
kuanzia saa 10 kwenye uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment