MGOMBEA Lina
Kessy leo ameweza kutetea nafasi yake ya Uenyekiti katika uchaguzi wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA)
unaliofanyika kwenye hoteli ya Midlands mjini Morogoro.
Akizungumza jijini Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura
alisema kuwa Lina amewashinda wenzake Isabela Kapera na Joan Minja katika
uchaguzi huo kwa kukusanya kura 25 kati ya 50 zilizopigwa, huku Isabela akipata
kura 13 na Joan 11.
Wambura alisema kuwa mgombea pekee
wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Rose Kissiwa aliweza kupita katika kinyanganyiro
hicho kwa kujikusanyia kura 35 huku 13
zikisema hakuna na kura 2 zikiharibika.
Ofisa huyo alisema kuwa Amina Karuma
ameshika nafasi ya Ukatibu mkuu na kumshinda mpinzani wake Cecilia Mkafum baada ya kupata kura 35 huku
mpinzani wake akipata kura 15.
Mwandishi mwaandamizi Zena Chande
ambaye alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo katika nafasi ya mjumbe wa
mkutano mkuu wa TFF aliweza kupata kura 24 huku kura 22 zikimkataa na 4 zimeharibika.
Hongera Amina. Mungu akupe nguvu, ujasiri na maarifa uweze kuikabili kazi iliyo mbele yako.
ReplyDelete