Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, January 31, 2013

WAKATI TUNISIA IKIAGA AFCON, TOGO YAONJA ROBO FAINALI



Mechi ya mwisho ya makundi kati ya Togo na Tunisia, moja ya mechi ngumu zaidi katika fainali za mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu imekamilika.
Timu hizo mbili zimetoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja na hivyo Togo imefuzu kutokana na idadi ndogo ya magoli waliyofungwa katika raundi hiyo ya kwanza, licha kuzoa alama nne sawa na Tunisia.
 
Tunisia ilihitaji ushindi katika mechi hiyo ili ifuzu kwa raundi ijayo huku togo nikihitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu kwa raundi ijayo.
Togo ilianza mechi hiyo kwa vishindo huku ikipata bao lake la kwanza kunako dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji Serge Gakpe ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wa timu hiyo Emmanuel Adebayor.
Kunako dakika ya 30 Tunisia ilizawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wake Walid Hichri kuangusha kwenye eneo la hatari na Dare Nibombe.

UHAMISHO WA DROGBA WAISHTUA SHANGHAI SHENHUA YASEMA HAIUTAMBUI


Uhamisho wa Didier Drogba kuelekea Galatasaray ya Uturuki uko mashakani kufuatia klabu yake ya Shanghai Shenhua kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo ana mkataba nao.
 
Galatasaray ilitangaza kumsaini Drogba jumatatu kwa mpango wa uhamisho wenye thamani ya euro milioni €6 mpaka kiangazi 2014.
Shenhua imesema imesema inajipanga kuweka pingamizi.

Taarifa iliyotolewa na Shenhua kupitia mtandao wa klabu hiyo ikisomeka "Klabu imeshtushwa sana. Drogba bado ni mchezaji wa Shanghai Shenhua kwa kuwa ana mkataba nasi nab ado yuko katika kipindi halali cha mkataba.

"Shanghai Shenhua iko tayari kuepeleka ushahidi FIFA ili kupinga jaribio hilo”

MGOMBEA SAID MOHAMED ANAYEGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA LIGI AONDOLEWA PINGAMIZI

Wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya shirikisho la soka nchini TFF na bodi ya ligi kuu ukizidi kupamba moto huku baadhi ya wagombea wakiwekewa mapingamiz na wadau mbalimbali wa soka nchi hatimaye pingamizi alilowekewa mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti Said Mohamed limeondolewa.

Pingamizi liliwekwa kwa mgombea huyo lilitoka kwa katibu wa zamani wa chama cha soka mkoa wa kisoka wa Kinondoni Frank Mchaki ambaye aliweka pingamizi hilo kutokana na kwamba mgombea huyo hakuwa kiongozi wa klabu yoyote nchini.

Hata hivyo kufuatia kamati ya uchaguzi kukutana na wagombea na wawekaji wa mapingamizi hayo kwa lengo la kufanyika mapitio ya mapingamizi mbalimbali na sababu za mapingamizi hayo imedhihika kuwa Mzee Said Mohamed ni kiongozi wa Azam fc kwa nafasi ya mwenyekiti.

Akiongea na waandhishi wa habari hii mwekaji wa pingamizi hilo Mchaki amesema ameridhishwa na zoezi la kuhakiki nafasi ya uongozi ya mzee Said Mohamed ndani ya Azam kwani aliweka pingamizi kwa kuwa alikuwa hana uhakika kama Said Mohamed ni kiongozi wa kuchaguliwa wa Azam licha ya kwamba amekuwa akisikia kuwa ni kiongozi wa klabu hiyo.

Mchaki amesema mzee Said Mohamed alikuja na vielelezo kamili ambavyo vimeonyesha kuwa alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti 1/10/2012 alikuwa ni mwenyekiti wa Azam.

Kumbuka moja ya sifa ya kuwania nafasi ya uongozi ndani ya bodi ya ligi, mgombea anapaswa kuwa kiongozi katika moja ya vilabu vya ligi kuu.

KLABU YA ASHANTI YAANZA VEMA MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA TAIFA

Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili.

Bondia Hamisi Matunda wa Klabu ya Mashine ya Maji kushoto akipambana na Abdallah Shamte wa Klabu Ya Ashanti ya ilala Shamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili


Bondia wa Klabu Ya Ashanti ya Ilala Abdallah Shamte akipambana na Hamisi Matunda wa Mashine ya maji wakati wa mashindano ya klabu bingwaShamte aliibuka na ushindi wa TKO raundi ya pili

Mashabiki wa ASHANTI BOXING YA ILALA WAKISHANGILIA

KOCHA MKUU WA TAIFA STARS KIM POULSEN ATANGAZA WACHEZAJI 21 WA KUIVAA CAMEROUN

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MBUNGE WA KINONDONI, IDD AZAN MGENI RASMI PAMBANO LA KASEBA NA MANENO


Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan.

MBUNGE wa Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idd Azan, amepangwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la Ubingwa wa Taifa, litakalowakutanisha Japhet Kaseba na Ramadhan Maneno, liliopangwa kufanyika Machi 2 mwaka huu, katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo ndilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa masumbwi, likiwakutanisha wakali wa ndondi, akiwamo Kaseba, aliyewahi kuwika pia kwenye ngumi za mateke.

Akizungumza na Lenzi ya Michezo Kaseba alisema kuwa pambano lao litahudhuriwa na mbunge wa Kinondoni, akiwa na shauku ya kutaka kujua nani mkali.

Alisema katika masumbwi hayo, kila mmoja anataka kuonyesha makali yake, huku yeye akiwa na hamu zaidi ya kuonyesha kwanini anakimbiwa na mabondia wengi.

“Nimekuwa nikikimbiwa sana na mabondia hapa nchini, hivyo naamini katika pambano hili ambalo mgeni rasmi atakuwa mbunge wa Kinondoni, nitaonyesha ukweli huo.

“Kila kitu kinaendelea vizuri kuelekea katika patashika hiyo itakayokutanisha pia mabondia wengine wenye uwezo, akiwamo Mtambo wa Gongo na wengineo,” alisema.

Mwaka jana Kaseba alishindwa kupigana na Francis Cheka, licha ya kutangazwa mno na wadau wa ngumi na kupangwa kufanyika katika Uwanja mpya wa Taifa

Wednesday, January 30, 2013

MASHINDANO YA NGUMI YA KLABU BINGWA TANZANIA KUANZA KESHO, MABONDIA WAPIMA UZITO


Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya ngome ambaye aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika London mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam Leo kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa ya Taifa yanayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa taifa


Bondia Abdallah Shamte wa Klabu ya Ashanti ya Ilala akipima uzito kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa yatakayoanza kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa

LULU AKIWA NA USO WA MACHOZI YA FURAHA BAADA YA KUACHIWA

Msanii  Elizabeth "Lulu" Michael tayari amerudi uraiani baada ya kuachiwa kwa dhamana katika mahakama kuu jijini Dar. Licha ya kukamilisha kwa masharti yote aliyopewa jana ikiwa ni pamoja na kutoa milioni 20 kwa wadhamini wawili, kuripoti kila mwanzo wa mwezi na kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo, Lulu hakufanikiwa kutoka kwa kile kilichoripotiwa kutokuwepo kwa msajili , hivyo kumlazimu kurudi gerezani

Lulu (katikati) akiwa mwenye majonzi na furaha hapa akitokwa na machozi wakati msemaji wa familia Msanii Dr Cheni akizungumza . Lulu amewaomba watanzania wote wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi yake bado inaendela.


LULU na Mama yake mzazi ndani ya gari tayari kwa safari ya kurudi nyumbani
Wakili wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza kwasababu case bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe tarehe ya Lulu kurudi mahakamani.

Monday, January 28, 2013

WEST BROM YAKATAA KUMUUZA ODEMWINGIE

 

Peter Odemwingie
 
West Brom, imekata ombi la pili kutoka kwa klabu ya Queen Park Rangers QPR la kutaka kumsajili mshambuliaji wake Peter Odemwingie.
Wiki iliyopita, West Brom ilikataa pendekezo la QPR, la kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni tatu.
‘‘ Nina uhakika kuwa klabu ya West Brom haitafurahishwa na uamuzi wetu. Sisi tuliwasilisha ombi letu na ombi hilo ambao lilikuwa siri likatangazwa . kwa hakika mchezaji huyo alikuwa na hamu ya kuhamia London na hivyo ndivyo tulivyokuwa tumepanga’’
Odemwingie, Odemwingine alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni mbili nukta tano kutoka kwa klabu ya Lokomotive Moscow, mwaka wa 2010
Siku ya Jumapili mchezaji huyo alichapisha taarifa kwa mtandao wake wa Twitter akisema kuwa yuko nyumbani mwake akijiliwaza.
Aliongeza kuwa amezimika kufuta baada ya ujumbe alizokujwa amechapishwa kwenye mtandao huo wa twitter.
Baada ya yale yaliyofutwa inasema, ‘‘ Msimu uliopita ni wakati ambao ningeliwasilisha ombi la kuhama. Nilikuwa nikitaka kuhamia klabu ya Rubin Kazan, na wakati huo nilifahamishwa kuwa kamwe sitaruhusiwa kukihama klabu hiyo’’
‘ ‘ nikawaza kuhusu Newcastle, vile vile nikaambia sitauzwa,Wigan matokeo yakawa hayo hayo’’
Wiki iliyopita alichapicha ujumbe unaoashiria kuwa amehuzunika sana na kile alichokitaja kama ukosefu wa heshima kutoka kwa wasimamizi wa klabu ya Westbrom.
Odemwingie alisema kuwa katika umri wake, huenda asipate nafasi nyingine kama hiyo kutokana na umri wake.

TASWA YAANZA MCHAKATO WA MWANAMICHEZO BORA 2012



CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeanza mchakato wa Tuzo kwa Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012.

Kama ilivyokuwa mwaka uliopita Kamati ya Utendaji ya TASWA imeamua suala la mchakato wa kuwapata wanamichezo hao lifanywe na kamati maalum nje ya Kamati ya Utendaji ya TASWA lengo ikiwa ni kupanua wigo na kuwashirikisha wadau wengi zaidi katika jambo hili nyeti.

Jukumu la Kamati ya Utendaji ya TASWA itakuwa ni kuhangaika na mambo ya wadhamini na masuala mengine yahusuyo sherehe hizo ambazo tunataka ziwe za aina yake.

Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji ya TASWA iliyokutana wiki iliyopita iliteua kamati maalum ya watu 11 kusimamia mchakato wa kuwapata wanamichezo hao, ambapo kamati hiyo inayotarajia kuanza vikao vyake Jumatano Januari 30, 2013 itakuwa chini ya uenyekiti wa mwanachama wa TASWA, Haji Manara.

Kamati ya Utendaji imemkabidhi jukumu Manara baada ya kujiridhisha pasi na shaka uzoefu wake katika masuala ya michezo na pia uzoefu wake katika mambo mbalimbali ya kiutawala, hivyo kuwa na imani kwamba ataendesha vizuri mchakato kama walivyofanya watangulizi wake.

Wajumbe saba wa kamati hiyo wanatoka nje ya Kamati ya Utendaji ya TASWA ambao ni Jane John, Dina Ismail, Jabir Idrissa, Tulo Chambo, Abdallah Mweri na ofisa mmoja ambaye ataombwa kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), wakati wajumbe wanne wanatoka Kamati ya Utendaji ya TASWA ambao ni Grace Hoka, Zena Chande, Alfred Lucas na Amir Mhando.

Imetolewa na:
Amir Mhando

NSA JOB ASIKITISHWA NA KITENDO CHA GOLIKIPA WA JKT RUVU PATRICK KUTOMJULIA HALI WALA KUMWOMBA MSAMAHA

Nsa job hajapokea hata ‘pole’ kutoka kwa Patrick, Kipa wa JKT Ruvu
Mshambuliaji hatari wa timu ya Coastal Union, Nsa Job, amesema anasikitishwa na kitendo cha kipa wa timu ya JKT Ruvu, Patrick, kutompigia simu wala kumuona hadi sasa.
Nsa alipata maumivu makubwa ya goti lake wakati alipogongana na kipa wa timu hiyo katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu katika uwanja wa Chamazi, Complex, Oktoba mwaka jana na kupelekea goti lake kuzunguka. Lakini baada ya kufanyiwa upasuaji uliokwenda vizuri nchini, India, mshambuliaji huyo wa zamani wa timu za Simba na Yanga, ameanza mazoezi na sasa ana matumaini ya kucheza soka kwa mara nyingine.


Nsa alipokuwa Hospitali
 
“Yule kipa wa JKT Ruvu, hajawahi kunipa pole wala kunijulia hali hadi sasa. Unajua nilikata tamaa ya kucheza tena soka nilipoona hali ya mguu wangu mara baada ya kuumia. Nilijua ndiyo mwisho wa kipaji changu, lakini sasa nafarijika na kujiona mwenye nguvu mpya baada ya kuanza mazoezi” anasema, mshambuliaji huyo mwenye mabao matatu hadi sasa.
 
” Narudi kivingine, waambie mashabiki kuwa narejea kwa nguvu na watarajie mambo mazuri kutoka kwangu”, Nsa anasemaje kuhusiana na mwenendo wa ligi kuu. ” Ligi imeingia katika kipindi ambacho kinachangamoto nyingi. Mimi nafikiri timu iliyofanya maandalizi mazuri ndiyo itapata matunda” anamaliza.
 
Ikumbukwe TFF waliomuomba radhi Nsa kwa kukosekana gari la wagonjwa wakati wa mchezo huo.
Coastal imeanza mzunguko wa pili kwa ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Mgambo FC kutoka Tanga.

ELIZABETH MICHAEL MAARUFU KAMA LULU AACHIWA KWA DHAMANA LEO, FAMILIA WAKAMILISHA MASHARTI KAZI KUPATA SAINI MBILI AMBAZO WAHUSIKA WAPO NJE YA MKOA KIKAZI, ALAZIMIKA KULALA TENA RUMANDE LEO


Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na kusalimisha kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja. Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba. (Picha na Habari Mseto Blog)


Lulu akipanga gari la magereza.




Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani leo


Lulu akisindikizwa na askari Magereza.


Lulu akiingia katika gari la Magereza kwenda Rumande

MSANII nyota wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael, maarufu kama (Lulu), ameachiwa kwa dhama leo katika Mahakama Kuu, mbele ya jaji, Zainabu Muruke.

Lulu alifikishwa mahakamani akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, ambaye hata hivyo baadaye alibadilishiwa kesi na kushitakiwa kwa kuua bila kukusudia.

Msanii huyo ameachiwa huku akipewa masharti ya kuacha Hati ya Kusafiria Mahakamani, kuripoti Mahakamani kila tarehe mosi, pamoja na wadhamini wawili waliotoa milioni 20 mmoja.

Kwa wiki kadhaa sasa, baadhi ya watu wamekuwa wakisikika wakiomba dua njema kwa msanii huyo ili aweze kuachiwa kwa dhamana na kufuatilia kesi yake akiwa nje na familia yake.

Lulu aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya dhamana, kupitia kwa jopo la mawakili wake, linaloongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala, Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Awali, maombi hayo ya dhamana yaliwasilishwa mahakamani hapo kwa hati ya dharura na kusikilizwa na jaji Zainabu Muruke.

Mara baada ya tukio la mauaji ya Kanumba kutokea, kesi ya msanii huyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Kisutu ili kukamilisha hatua za awali, hasa masuala yote ya kisheria, upelelezi na kushtakiwa kwa mauaji ya kuua bila kukusudia kwa kupitia Kifungi cha 196.

Kesi ya Lulu yenye namba 125, jalada lake lilifungwa na kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa kuwa ndiyo yenye uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Mara baada ya kufika mahakamani hapa leo asubuhi, dalili njema za kuachiwa kwa msanii zilianza kujitokeza hasa baada ya dhamana yake kuwa wazi, ikiwa ni kutokana na hoja zilizokuwa zinajadiliwa mahakamani hapo.

Katika mitandao ya kijamii, ikiwamo facebook, baadhi ya watu walionekana wakipost habari na picha mbalimbali za msanii huyo zikionyesha dhahiri kumuombea mema ili atoke na kuendelea na maisha yake wakati kesi hiyo inaendelea.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wa kike wenye mvuto mkubwa katika jamii, huku uwezo wake na umahiri wake wa uigizaji ukiacha watu midomo wazi.

Umaarufu wa Lulu ulitokea tangu mdogo akiigiza katika kundi la Kaole Sanaa Group, akicheza kama mt0to hadi kufikia kuwa msichana na mwenye mvuto miongoni mwa mabinti wa filamu Tanzania.

Bila shaka habari za kuachiwa kwa dhamana kwa msanii huyo zitakuwa njema kwa siku ya leo kwa mashabiki na wadau wote wa filamu Tanzania.

Hata hivyo Lulu atalazimika kusubiri hati ya mahakama isainiwe na wafanyakazi wawili wa mahakama ambao inasemekana wapo mkoani Pwani kikazi hivyo huenda akalazimika kuendelea kulala gerezani hadi kesho.

MECHI YA YANGA NA TANZANIA PRISON YAINGIZA MILIONI 101

Yanga na Tanzania Prisons zimeingiza mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).
Mechi hiyo namba 94 ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Watazamaji 16,158 kati ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ni 98 waliokata tiketi za sh. 20,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na gharama za tiketi ni sh. 12,363,433.45.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 7,413,060.07, Kamati ya Ligi sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

Sunday, January 27, 2013

CAPE VERDE YAFUZU ROBO FAINALI AFCON, YAIFUNGA ANGOLA 2-1


Timu ya taifa ya Cape Verde

Cape Verde imeandikisha historia nyingine kwa kufuzu kwa robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika baada ya kuibanjua Angola kwa magoli mawili kwa moja.
Cape Verde ambayo inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza ilitoka nyuma ya kufungwa bao moja kwa bila na Angola na kuandikisha ushindi wao wa kwanza katika fainali hizo.
Cape imemaliza na alama tano sawa na Afrika Kusini lakini ikizidiwa na wingi wa magoli.
Mshambulizi wa ziada Heldon, ndiye aliyeifungia Cape Verde bao lake la ushindi kunako dakika ya tisini ya mechi hiyo.

Angole ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kunako dakika ya 36 baada ya mchezaji wa Cape Verde kujifunga mwenyewe lakini vijana hao wa cape Verde walisawazisha kunako dakika ya 81 kupitia kwa mshambuliaji wake Varel.

Morocco nayo imeyaaga mashindano hayo katika raundi ya makundi sawia na Angola ambayo ilizoa alama mbili na moja mtawalia.
Kinyume na ilivyokuwa katika mechi kati ya Afrika Kusini na Morocco ni mashambiki wachache sana walihudhuria mechi hiyo na ushindi wa Afrika Kusini katika mechi yao ya mwisho huenda ukachochea mashabiki zaidi kufika katika viwanja mbali mbali wakati wa mechi ya robo fainali.

Cape Verde sasa inajumuika na Afrika Kusini na Ivory Cost ambayo tayari zimejikatia tikiti ya robo fainali ya mashindano hayo, yanayoendekea nchini Afrika Kusini.
Wawakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, leo inajitosa uwanjani kucheza mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Mali, mechi ambayo ni sharti washinde ili wafuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

LIVERPOOL YANYUKWA NA OLDHAM YA DARAJA LA KWANZA , YAAGA RASMI FA


Wachezaji wa Livepool wakicheza na Leeds

Tottenham imebanduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la FA baada ya kulazwa magoli mawili kwa moja na Leeds United.
Luke Varney aliifungia Leeds bao lake la kwanza kabla ya Ross McCormack, kufunga la pili. Tottenham ambayo inashiriki katika ligi kuu ya Premier nayo ikapata bao lake kupitia kwa mchezaji wake Clint Dempsey.
Katika mechi nyingine Chelsea, nusura iage mashindano hayo baada ya kulemewa na Bendford.
Hata hivyo Fernando Torres aliifungia Chelsea bao lake la pili na kuiepushia aibu kubwa.
Wachezaji wa Leeds
Timu hizo mbili zilitoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili.
Liverpool vile vile, imeondolewa kwenye michuano hiyo ya FA, baada ya kunyukwa magoli 3-2 na Oldham, ambayo inashiriki katika ligi daraja ya kwanza.
Timu zingine za ligi kuu ambazo zimefuzu kwa raundi ijayo ni pamoja na Manchester United, Everton, Arsenal, Wigan, reading na Manchester City.
Norwich, QPR na stoke city zinaungana na timu ambazo zimefunganya

HUKUMU YA KIFO KWA WATU 21 YA MAHAKAMA NCHINI MISRI YASABABISHA VURUGU TENA, WACHEZAJI WAWILI WAPOTEZA MAISHA

WADAU wa soka nchini Misri wako katika maombolezo baada ya mchezaji wa Marek Mahmoud Abd Al Halem na golikipa wa zamani wa Al Masry, Tamer Fahalawas kuuwawa katika vurugu zinazoendelea huko Port Said.

Watu zaidi ya 30 wameuwawa Port Said kuanzia jumamosi katika mapigano ya waandamanaji na vikosi vya usalama vya eneo hilo, vurugu ambazo zilizuka baada ya Mahakama nchini humo kuwahukumu kifo watu 21 ambao walihusika katika vurugu zilizoua watu 74 katika mchezo wa soka kati ya Al Masry na Al Ahly.

Mashabiki wa timu zote mbili ambao wanajulikana kama Ultras wanadai kuwa polisi nao walihusika kwa kiasi kuchangia vifo vilivyotokea Port Said na kumlaumu rais wa Misri Mohammed Morsi kwa kushindwa kulisuka upya jeshi hilo.

Mwenyekiti wa Merekh Morsy Sarhan alithibitisha kifo cha Abd Al Halem ambaye alijiunga na timu hiyo miezi michache iliyopita ambapo tukio hilo lilimkuta wakati akielekea mazoezini. Sarhan aliongeza kuwa wataomboleza kifo cha mchezaji huyo kwa siku tatu ambaye alipigwa risasi pamoja na kutokuwa na hatia na kuwataka watu kuheshimu maamuzi ya mahakama ili maisha ya mchezo wa soka nchini humo yarejee kama kawaida.

WASANII WA BONGO MOVIE WAPAGAWISHA MASHABIKI DAR LIVE

Kundi la Scorpion Girls likiongozwa na Isabela Mpanda (katikati) likiporomosha burudani wakati wa Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Mrembo Jacqueline Wolper akiwapa 'hi' mashabiki.

Jacob Steven 'JB' akionyesha umahiri wake wa kusakata rhumba wakati wa tamasha hilo.

Steve Nyerere naye akionyesha manjonjo yake stejini.

Mastaa wa filamu wakiwa jukwaani kuwasalimia mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.


Snura Mushi akiwapagawisha mashabiki.

Msanii Afande Sele akiwarusha mashabiki ndani ya Dar Live.

Tundaman akiwachizisha mashabiki.

...akizidi kuwapa raha mashabiki.

Kingwendu akifanya vitu vyake.

Richie naye akionyesha ufundi jukwaani.

Dk. Cheni na mwanadada wakienda sambamba.

Shamsa Ford akisema na mshabiki.

Bi. Mwenda akiwa kapagawa na shangwe za Dar Live.

Mrisho Mpoto akiwapa raha mashabiki.

Afande Sele akiwapa 'hi' mashabiki.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo ambaye pia ni Meya wa Ilala, Mhe. Jerry Slaa akiwasabahi mashabiki.

Nyomi iliyohudhuria tamasha hilo.

Afande Sele akiwa amebebwa na mashabiki.

Bi. Mwenda akionyesha machejo yake stejini.

Ilikuwa ni full burudani ndani ya Dar Live.

Scorpion Girls wakizidi kupagawisha.

Snura na wanenguaji wake wakilishambulia jukwaa.

Bendi ya Twanga Pepeta ikitoa burudani katika Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Shilole akiwapa raha mashabiki.

Burudani zikiwa zimepamba moto mahali hapo.

Wanenguaji wa Shilole wakimpagawisha shabiki aliyepanda jukwaani.

Raha zikizidi kushamiri mahali hapo.

Baadhi ya mastaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Jerry Slaa (katikati).

Sabrina Rupia ‘Cathy’ katika pozi.

Baadhi ya mastaa wa filamu wakiwa katika picha ya pamoja na rais wao Mwakifwamba (wa pili kulia).

Mrisho Mpoto akiwa katika pozi.

Tundaman akipozi katika Red Carpet.

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba katika pozi.

Jack Wolper katika pozi.

Mrembo Rose Ndauka katika pozi.

Kingwendu akipozi na watoto katika Red Carpet.

Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam limeacha historia baada ya kutawaliwa na burudani za kila aina kutoka kwa wasanii wa filamu na wale wa Bongo Fleva. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyochukua nafasi wakati wa tamasha hilo. (PICHA ZOTE: ERICK EVARIST NA MUSA MATEJA/GPL)