Msanii wa filamu
nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi
rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya
dhamana ikiwa ni pamoja na kusalimisha kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya
kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa
msajili kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa
serikali ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake
marehemu Steven Kanumba. (Picha na Habari Mseto Blog)
Lulu akipanga gari la
magereza.
Gari lililomleta Lulu
likiondoka mahakamani leo
Lulu akisindikizwa na askari
Magereza.
Lulu akiingia katika gari la
Magereza kwenda Rumande
MSANII
nyota wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael, maarufu kama (Lulu), ameachiwa
kwa dhama leo katika Mahakama Kuu, mbele ya jaji, Zainabu Muruke.
Lulu
alifikishwa mahakamani akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba,
ambaye hata hivyo baadaye alibadilishiwa kesi na kushitakiwa kwa kuua bila
kukusudia.
Msanii
huyo ameachiwa huku akipewa masharti ya kuacha Hati ya Kusafiria Mahakamani,
kuripoti Mahakamani kila tarehe mosi, pamoja na wadhamini wawili waliotoa
milioni 20 mmoja.
Kwa
wiki kadhaa sasa, baadhi ya watu wamekuwa wakisikika wakiomba dua njema kwa
msanii huyo ili aweze kuachiwa kwa dhamana na kufuatilia kesi yake akiwa nje na
familia yake.
Lulu
aliwasilisha mahakamani hapo maombi ya dhamana, kupitia kwa jopo la mawakili
wake, linaloongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala, Fulgence
Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Awali,
maombi hayo ya dhamana yaliwasilishwa mahakamani hapo kwa hati ya dharura na
kusikilizwa na jaji Zainabu Muruke.
Mara
baada ya tukio la mauaji ya Kanumba kutokea, kesi ya msanii huyo ilifunguliwa
katika Mahakama ya Kisutu ili kukamilisha hatua za awali, hasa masuala yote ya
kisheria, upelelezi na kushtakiwa kwa mauaji ya kuua bila kukusudia kwa kupitia
Kifungi cha 196.
Kesi
ya Lulu yenye namba 125, jalada lake lilifungwa na kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa
kuwa ndiyo yenye uwezo wa kusikiliza
kesi za mauaji.
Mara
baada ya kufika mahakamani hapa leo asubuhi, dalili njema za kuachiwa kwa msanii
zilianza kujitokeza hasa baada ya dhamana yake kuwa wazi, ikiwa ni kutokana na
hoja zilizokuwa zinajadiliwa mahakamani hapo.
Katika
mitandao ya kijamii, ikiwamo facebook, baadhi ya watu walionekana wakipost
habari na picha mbalimbali za msanii huyo zikionyesha dhahiri kumuombea mema ili
atoke na kuendelea na maisha yake wakati kesi hiyo inaendelea.
Lulu
ni miongoni mwa wasanii wa kike wenye mvuto mkubwa katika jamii, huku uwezo wake
na umahiri wake wa uigizaji ukiacha watu midomo wazi.
Umaarufu
wa Lulu ulitokea tangu mdogo akiigiza katika kundi la Kaole Sanaa Group,
akicheza kama mt0to hadi kufikia kuwa msichana na mwenye mvuto miongoni mwa
mabinti wa filamu Tanzania.
Bila
shaka habari za kuachiwa kwa dhamana kwa msanii huyo zitakuwa njema kwa siku ya
leo kwa mashabiki na wadau wote wa filamu Tanzania.
Hata hivyo Lulu atalazimika kusubiri hati ya mahakama isainiwe na wafanyakazi wawili wa mahakama ambao inasemekana wapo mkoani Pwani kikazi hivyo huenda akalazimika kuendelea kulala gerezani hadi kesho.
Hata hivyo Lulu atalazimika kusubiri hati ya mahakama isainiwe na wafanyakazi wawili wa mahakama ambao inasemekana wapo mkoani Pwani kikazi hivyo huenda akalazimika kuendelea kulala gerezani hadi kesho.
No comments:
Post a Comment