Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, January 28, 2016

TFF YAZIOMBA RADHI KLABU ZA LIGI KUU



RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi ameomba radhi klabu 15 na wadau wa soka kwa ujumla kufuatia sakata la ruhusa ya Azam FC kwenda kucheza mechi za kirafiki Zambia na kuahirishiwa baadhi ya michezo yao ya ligi.
Akizungumza kwa masikitiko, Malinzi alisema kuondoka kwa Azam FC, wakati ligi ikiendelea ni jambo ambalo haliwezi kuvumilika endapo tunahitaji kuwa na ligi bora ambayo ina ushindani.
“Ndugu zangu mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na siyo kukimbia akiwa uchi, hivyo na mimi kwa unyenyekevu naomba radhi timu zote 15 na wadau wa soka na kuwahakikishia kuwa haki itatendeka”, alisema Malinzi.
Pia alisema kuondoka kwa Azam FC, hataweza kusababisha kupanga matokeo badala yake watajiumiza wenyewe kwani watalazimika kucheza mechi mbili au tatu kwa wiki ili kwenda sambamba na wengine.
“Kuondoka kwa Azam FC, kunaiathiri wenyewe kwani watajikuta hawapati mapumziko ya kutosha (match recovery) kwa vile watalazimika kucheza michezo miwili au mitatu kwa wiki ili kuzipa pengo na pia watakuwa kwenye maandalizi ya Kombe la Shirikisho”, alisema Malinzi.
Hatua hii ya Malinzi imekuja baada ya klabu za Ligi Kuu kupinga hatua ya kuwapa ruhusa Azam FC kwenda kucheza mechi za kirafiki na kuahirishiwa baadhi ya michezo yao ya Ligi, kitu ambacho Simba walilazimika kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari wakihofu kuwa kuahirishwa kwa mechi hizo kunaweza kutengeneza mazingira ya kupanga matokeo.
Azam FC imekwenda Zambia kushiriki michuano maalumu inayoshirikisha timu nne, iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa klabu mbili za huko, Zesco United na Zanaco FC, yaliyoanza kutimua vumbi juzi ndani ya Uwanja wa Levy Mwanawasa jijini Ndola nchini humo.
Timu nyingine mwaliko ni Chicken Inn ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment