West Brom, imekata ombi la pili kutoka kwa klabu ya Queen Park
Rangers QPR la kutaka kumsajili mshambuliaji wake Peter Odemwingie.
Wiki iliyopita, West Brom ilikataa pendekezo la QPR, la kutaka kumsajili
mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni tatu.
Akiongea na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, kocha wa QPR, Harry
Redknapp, amesema kwa sasa wanakabiliwa na wakati mgumu na kuwa mambo mengi
yamekwenda kinyume na matarajion yao.
‘‘ Nina uhakika kuwa klabu ya West Brom haitafurahishwa na uamuzi wetu. Sisi
tuliwasilisha ombi letu na ombi hilo ambao lilikuwa siri likatangazwa . kwa
hakika mchezaji huyo alikuwa na hamu ya kuhamia London na hivyo ndivyo
tulivyokuwa tumepanga’’Odemwingie, Odemwingine alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni mbili nukta tano kutoka kwa klabu ya Lokomotive Moscow, mwaka wa 2010
Siku ya Jumapili mchezaji huyo alichapisha taarifa kwa mtandao wake wa Twitter akisema kuwa yuko nyumbani mwake akijiliwaza.
Aliongeza kuwa amezimika kufuta baada ya ujumbe alizokujwa amechapishwa kwenye mtandao huo wa twitter.
Baada ya yale yaliyofutwa inasema, ‘‘ Msimu uliopita ni wakati ambao ningeliwasilisha ombi la kuhama. Nilikuwa nikitaka kuhamia klabu ya Rubin Kazan, na wakati huo nilifahamishwa kuwa kamwe sitaruhusiwa kukihama klabu hiyo’’
‘ ‘ nikawaza kuhusu Newcastle, vile vile nikaambia sitauzwa,Wigan matokeo yakawa hayo hayo’’
Wiki iliyopita alichapicha ujumbe unaoashiria kuwa amehuzunika sana na kile alichokitaja kama ukosefu wa heshima kutoka kwa wasimamizi wa klabu ya Westbrom.
Odemwingie alisema kuwa katika umri wake, huenda asipate nafasi nyingine kama hiyo kutokana na umri wake.
No comments:
Post a Comment