WADAU wa soka nchini Misri wako
katika maombolezo baada ya mchezaji wa Marek Mahmoud Abd Al Halem na golikipa wa
zamani wa Al Masry, Tamer Fahalawas kuuwawa katika vurugu zinazoendelea huko Port
Said.
Watu zaidi ya 30
wameuwawa Port Said kuanzia jumamosi katika mapigano ya waandamanaji na vikosi vya
usalama vya eneo hilo, vurugu ambazo zilizuka baada ya Mahakama nchini humo
kuwahukumu kifo watu 21 ambao walihusika katika vurugu zilizoua watu 74 katika
mchezo wa soka kati ya Al Masry na Al Ahly.
Mashabiki wa timu zote mbili ambao
wanajulikana kama Ultras wanadai kuwa polisi nao walihusika kwa kiasi kuchangia
vifo vilivyotokea Port Said na kumlaumu rais wa Misri Mohammed Morsi kwa
kushindwa kulisuka upya jeshi hilo.
Mwenyekiti wa Merekh Morsy Sarhan
alithibitisha kifo cha Abd Al Halem ambaye alijiunga na timu hiyo miezi michache
iliyopita ambapo tukio hilo lilimkuta wakati akielekea mazoezini. Sarhan aliongeza kuwa wataomboleza kifo
cha mchezaji huyo kwa siku tatu ambaye alipigwa risasi pamoja na kutokuwa na
hatia na kuwataka watu kuheshimu maamuzi ya mahakama ili maisha ya mchezo wa
soka nchini humo yarejee kama kawaida.
No comments:
Post a Comment