Miss Grand Tanzania, Jihan Dimack aiweka ramani ya Tanzania peupeeee
MISS Grand Tanzania, Jihan Dimack ameendelea kung’ara kwa kuonesha umahiri wake katika kipengele cha vazi la taifa wakati wa fainali za Miss Grand International 2026.
Jihan alivaa vazi linaloonesha utajiri na utamaduni wa Tanzania, likiwa na mchanganyiko wa mavazi ya Kimasai, wanyama wa porini na majengo ya kihistoria ya Zanzibar.
Muonekano wa vazi lake ulikuwa wa wanyama maarufu na vivutio vya Serengeti kama vile twiga na pundamilia na mchanganyiko wa kitamaduni ukionesha maisha ya Wamasai (akiwemo mwanamke aliyembeba mtoto mgongoni) na urithi wa Waswahili.
Michoro au miundo inayowakilisha majengo ya kihistoria ya visiwa vya Zanzibar pamoja na nyumba za asili za makuti na mapambo yanayoashiria madini ya kipekee ya tanzanite na vito vingine vya thamani vinavyopatikana nchini.
Wakati akipita jukwaani kuonesha vazi hilo Jihan alionesha kujiamini huku akitembelea kwa madaha mithili ya twiga hali iliyozidisha urembo wake.
Hivi sasa Jihan ameingia katika hatua ya tatu bora katika kipengele cha nguvu ya nchi akichuana na wawakilishi kutoka Ecuador na Vietnam, na washiriki wawili pekee wakitarajiwa kufuzu hatua inayofuata.
Mshindi wa kipengele hicho atapata nafasi ya moja kwa moja ya kuwa miongoni mwa warembo 20 bora wa shindano hilo linalofanyika Thailand na fainali zitafanyika Jumamosi.
Post a Comment