WABUNGE WAPITISHWA MAFUNZO YA MAONI YA WATOTO DIRA 2050
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Daniel Sillo amefungua mafunzo ya kuwapitisha wabunge kuhusu maoni ya yaliyotolewa na watoto katika Dira ya Taifa ya 2050.
Mafunzo hayo yamefanyika Oktoba 31, 2026 Bungeni jijini Dodoma yakiwahusisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Kamati ya Ufuatiliaji na Tathimini pamoja na Kikundi cha Wabunge cha Maendeleo ya Awali ya Mtoto.
Akizungumzia maoni yaliyotolewa, mmoja wa watoto aliyeshiriki kutoa maoni hayo Raphael Charles ameishukuru Serikali kwa kutambua umuhimu wa maoni ya watoto katika Dira ya 2050 ambapo jumla ya watoto 14,000 walisikilizwa maoni yao kutoka Zanzibar na Mikoa mitatu ya Tanzania Bara nchini.
Amesema watoto ndio watakaonufaika na Dira ya 2050 hivyo ni muhumu maoni yao yalivyosikilizwa.
Mtoto huyo amesema wakati wa kukusanya maoni yao watoto wengi walitoa maoni katika sekta ya elimu, afya, lishe, upatikanaji wa maji safi na salama, ulinzi wa mtoto pamoja na ushirikishwaji wa mtoto.
Kwa upande wao, Waheshimiwa Wabunge wamesisitiza Serikali kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na watoto ikiwemo kuboresha lishe mashuleni, kutokomeza ukatili wa mtoto na kubadilisha Sheria ya Ndoa.
Mafunzo hayo yametolewa chini ya Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP III) unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP).
Post a Comment