MARAIS WAWILI WAZINDUA MJI WA SERIKALI MTUMBA

 



 Historia mpya imeandikwa leo, Oktoba 30, 2026, baada ya Mji wa Serikali Mtumba kuzinduliwa rasmi Jijini Dodoma, ikiwa ni utimizaji wa ndoto ya miaka 53 iliyobuniwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1973.

Hafla hiyo ya kishindo imeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akishirikiana na mgeni wake wa kitaifa, Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço.

Marais hao wawili wameshirikiana kuvuta kitambaa na kukata utepe kuashiria ufunguzi wa majengo ya kisasa ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali, pamoja na miundombinu ya barabara za lami ndani ya Mji huo wa Serikali.

Wakizungumza na viongozi pamoja na wananchi waliofurika katika Uwanja wa Mashujaa Mtumba, viongozi hao wameeleza kuwa mradi huo ni kielelezo cha ustawi, maendeleo, na utekelezaji wa maono ya muda mrefu ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu halisi ya nchi.

Mtumba sasa inasimama sio tu kama makao makuu ya utawala, bali kama Kioo Akisi cha Tanzania katika mpangilio wa mji wa kisasa na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.





































No comments