Jihan Dimachk Aivika Tanzania Taji la Dunia la Miss Grand International 2026

 


 


MREMBO Jihan Mohin Dimachk, kutoka Tanzania amevunja mwiko wa miaka mingi na kuandika rekodi ya kimataifa kama mwanamke wa kwanza kabisa kutoka bara la Afrika kutwaa taji Miss Grand International 2026 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2013.

Jihan alivikwa taji hilo katika ukumbi wa MGI Hall jijini Bangkok, Thailand

Kiukweli usiku wa Oktoba 10, 2026 utabaki umechorwa kwa wino wa dhahabu katika vitabu vya historia ya urembo duniani, baada ya binti huyo  kupata ushindi ambao si wa kubahatisha, huku akiwa anaungwa mkono na watuj wa nyumbani kwake.

 Jihan alishiriki katika katika high tempo akionesha uwezo wa juu, ujasiri, haiba ya kuvutia na akili ya kipekee iliyowafunika kabisa warembo wenzake 76 kutoka pande zote za dunia.

Katika kinyang'anyiro hicho kilichoshirikisha washiriki 77, Jihan alipambana kwa ustadi wa hali ya juu hatua kwa hatua, akipenya kutoka top 25 hadi kuingia top 5 ya mwisho ambapo alimwaga cheche na kuwafanya majaji wasiwe na mashaka yoyote kumkabidhi taji hilo kuu na kumvisha taji la ubingwa wa dunia.

Pambano hilo la kukata na shoka lilishuhudia Jihan akiwabwaga wapinzani wake wakali na kuacha nyuma mataifa makubwa ya urembo, ambapo Shyare Andrade kutoka Ecuador aliibuka mshindi wa pili yaani First Runner-Up, huku Beau Megan Goos wa Uholanzi akichukua nafasi ya tatu. Ximena Carrillo kutoka Guatemala alishika nafasi ya nne na Emoura Phạm wa Vietnam akafunga safu ya tano bora, huku warembo wengine kutoka Ivory Coast, Cuba, Mexico, Puerto Rico, Thailand na Venezuela wakiishia nafasi za tano bora za nyongeza.

Ushindi huu wa kihistoria umeilipua Tanzania na Bara zima la Afrika kwa furaha na fahari isiyo kifani, ukithibitisha kuwa urembo, uwezo na sauti ya mwanamke wa Kiafrika vina nguvu ya kutawala na kuongoza jukwaa la dunia.

Jihan Dimachk ameweka rasmi jina la Tanzania katika kilele cha urembo ulimwenguni, akionyesha kwa vitendo kuwa ndoto za binti wa Kitanzania hazina mipaka inapofikia kupambana na kuibuka kidedea kimataifa.

No comments