TUNAPOTEZA WATOTO KWA KUKOSA MALEZI






Makamu wa Rais Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amewataka Wazazi na Walezi kuzingatia malezi ya watoto kwa kuwajengea misingi ya kumpenda Mungu, kufanya kazi na kusoma.

Akizungumza katika Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema-Tabata Kimanga, Dar es salaam, Nchimbi alisema jamii inapoteza eneo kubwa katika malezi ya watoto wa siku hizi.
Amesema Watoto wanapaswa kufundishwa kumpenda Mungu, kufanya kazi na kusoma, akisema baadhi yao wamejikita zaidi katika michezo ya mtandaoni badala ya masomo.
“Kanuni kuu tatu, sala, kazi na masomo, tuwafanye watoto wajue na kumpenda Mungu, tufanye Watoto wetu wapende kufanya kazi, siku hizi Watoto wengi wanapenda game hivyo tuwafanye wapende kusoma kwani kutosoma kunawafanya wapende njia za mkato,” amesema Nchimbi.
Aidha, amesema serikali itaendelea kuthamini mchango wa taasisi za dini katika jamii.

No comments