TAMASHA LA KIZIMKAZI NI NGUZO YA UMOJA, MSHIKAMANO NA UDUGU WA KITAIFA
Tamasha la
Kizimkazi lililofanyika Zanzibar limetajwa kuwa jukwaa muhimu la kukuza umoja,
mshikamano wa kitaifa, na udugu wa kudumu miongoni mwa Watanzania huku likiimarisha
tunu ya Muungano .
Akizungumza
kufuatia kufungwa kwa tamasha hilo, Mtaalam wa Maridhiano, Amani na Maendeleo,
Dkt. Dennis Muchunguzi, aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli
mbalimbali za maendeleo ili kuchochea malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo
2050 na kulinda amani ya nchi.
Aidha, aliongeza
kuwa uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania Bara na Zanzibar una mizizi mirefu
hata kabla ya Muungano, akitolea mfano wa mchezo wa soka kati ya timu za Simba
na Yanga uliochezwa visiwani humo kama ushahidi wa mshikmano huo imara
unaopaswa kulindwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Dkt. Muchunguzi amesisitiza
kuwa mshikamano wa kitaifa ni msingi muhimu wa utekelezaji wa Dira ya Taifa
2050, hususan katika juhudi za kuinua uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Post a Comment