Simba Queens yatikisa Kigali




SIMBA Queens imeanza vema michuano ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake baada ya kuifunga Top Girls Academy FC ya Burundi mabao 2-0. Katika mchezo huo wa Baraza la Vyama vya Mpira kwa ushindi wa mabao 11-0 dhidi ya FC Ujeco. wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) uliochezwa Uwanja wa Pele Kigali, Simba Queens mabingwa wa 2022 walianza kufunga mabao yao kipindi cha pili baada Diafra Asha wa Top Girls Academy FC kukosa penalti.

Bao la kwanza la Simba Queens lilifungwa na Aisha Mnunka baada ya kuwazidi mbio mabeki na kumvisha kipa kanzu na mpira kujaa wavuni na bao la pili likafungwa na Musakanda Kusamula aliyeingia kipindi cha pili.

Katika mchezo wa mapema, Benki ya Biashara ya Ethiopia WFC (CBE) imeanza kwa ushindi wa mabao 11-0 dhidi ya FC Ujeco.

Katika michuano hiyo bingwa atawakilisha Kanda ya Cecafa kwenye Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) 2026. 

Mchezo wa pili Simba Queens watacheza kesho na Polisi Kenya.

Hii ni mara ya tatu Simba Queens ikifuzu michuano ambapo mara ya kwanza ni mwaka 2022 ilipotwaa ubingwa na kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Morocco.

Waliweka historia nyingine kwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Afrika mwaka 2024 iliyofanyika Ethiopia na kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kenya Police Bullets na kumaliza katika nafasi ya nne baada ya kufungwa mabao 2-0 na Kawempe Muslim ya Uganda, katika mchezo wa kusaka nafasi ya tatu.

Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za Kundi A ambapo vinara Yei Joint Stars watacheza dhidi ya Mafunzo Women (Zanzibar), huku Denden FC (Eritrea) wakimenyana na Rayon Sports WFC.

No comments