'WANAHUKUMIWA KWA CHUKI KASIMAMIE HAKI'

Rais Samia Suluhu Hassan akimwapisha Nalasco Kipanda kuwa Katibu wa Tume ya Maadili



Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jacob Kipanda kutoa maamuzi kwa misingi ya haki, akisema bado kuna Watumishi wanaohukumiwa kwa chuki na kupewa adhabu zisizoendana na makosa yao.
Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 1, 2026, Ikulu Jijini Dar es salaam, wakati akimuapisha Kipanda pamoja na Viongozi wengine wawili. Amesema Tume ya Watumishi wa Umma ina jukumu kubwa la kushughulikia mashauri ya Watumishi, yakiwemo malalamiko na migogoro, hivyo ni muhimu kuhakikisha haki inatendeka wakati wote.

“Huku kuna kazi kidogo kuna malalamiko, migogoro, uadilifu na hakikisha tume yako inasimamia haki, simamia tume iondoshe malalamiko kwa Watumishi”

“Pia migogoro ndani ya taasisi zetu kuna mambo mengi, Mtumishi anaweza akahukumiwa kwa chuki tu, kwa tatizo dogo lakini akapewa hukumu kubwa,” amesema Rais Samia.

No comments