UTEKELEZAJI DIRA 20250 WAANZA LEO
Safari ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 imeanza rasmi leo Julai 1, 2026, ikiwa ni hatua ya kugeuza maono ya maendeleo ya muda mrefu kuwa vitendo baada ya kuzinduliwa na Samia Suluhu Hassan Julai 17, 2025 jijini Dodoma.Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. Tausi Kida amesema kuanza kwa utekelezaji wa Dira hiyo kunahitimisha kipindi cha maandalizi na kufungua safari mpya ya miaka 25 ya kuleta mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia nchini.
Dk Kida amesema Dira ya 2050 imejengwa katika ushiriki wa wananchi wote, akisisitiza kuwa mafanikio yake yatategemea namna sekta za umma na binafsi zitakavyoingiza vipaumbele vya Dira hiyo katika shughuli zao za kila siku.
Dira ya 2050 inalenga kujenga taifa jumuishi, lenye ustawi, haki na linalojitegemea, huku ikitarajia kufikisha uchumi wa Tanzania kwenye thamani ya dola za Marekani trilioni moja na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja hadi dola za Marekani 7,000 ifikapo mwaka 2050.
.jpg)
Post a Comment