'SALUNI SIO UMBEYA'



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewataka wamiliki na Wafanyakazi wa saluni Nchini kuacha kuamini ushirikina na kujiepusha na umbea, badala yake wamtumainie Mungu na kudumisha amani katika maeneo yao ya kazi.

Makonda ameyasema hayo Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Chama cha Salonist Tanzania, akisema Sekta ya Urembo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na inaweza kuongeza tija zaidi endapo itawezeshwa ipasavyo.

“Ninawasihi mnaofanya kazi saluni muache ushirikina, mkaribisheni Mungu muone ufalme wake, mtunze amani kwenye saluni zenu, ziwe sehemu zinazohubiri amani, siyo kila mtu anapenda stori za kumjadili mwenzake,” amesema Makonda.

Aidha, Makonda amesema Serikali ina dhamira ya kuendelea kuiwezesha Sekta ya Urembo ili izidi kuchangia maendeleo ya uchumi na ajira. Kutokana na hilo, ameahidi kuwasilisha ombi rasmi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuongeza nguvu ya kifedha kwa wizara husika na kuhakikisha mifuko ya mikopo ya Serikali inawafikia kwa wingi Wamiliki na Wafanyakazi wa saluni.

No comments