CAF YAANDIKA HISTORIA KOMBE LA DUNIA
Afrika imeandika historia katika Kombe la Dunia 2026 baada ya timu tisa kati ya 10 zilizoiwakilisha bara hilo kufuzu hatua ya 32 bora, rekodi inayoonesha kuimarika kwa ushindani wa soka la Afrika dhidi ya mataifa makubwa duniani.Timu zilizofuzu ni Morocco, Senegal, Algeria, Misri, Ghana, Afrika Kusini, DR Congo, Cape Verde na Ivory Coast.
Baadhi zilimaliza zikiwa vinara wa makundi yao, huku nyingine zikifuzu kwa kuonesha kiwango cha juu, nidhamu na kujiamini.
Mafanikio hayo yanakuja baada ya Morocco kuweka historia katika Kombe la Dunia la 2022 kwa kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua ya nusu fainali, jambo lililoongeza imani kuwa timu za bara hilo zina uwezo wa kutwaa mafanikio makubwa zaidi.
Ni Tunisia pekee iliyoshindwa kuvuka hatua ya makundi.

Post a Comment