TUTAILINDA NCHI KWA NGUVU KUBWA



Serikali imepiga marufuku mikutano yote ya hadhara ya vyama vya siasa katika kipindi hiki, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na matishio ya uvunjifu wa amani na maandamano haramu yanayoratibiwa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii.

Akitoa taarifa bungeni jijini Dodoma leo Juni 26, 2026, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camillus Wambura, kusitisha utoaji wa vibali vya mikutano ya hadhara ili kuruhusu vyombo vya usalama kushughulikia vitisho vya uvunjifu wa amani vinavyotolewa nchini.

Aidha, ameagiza kufungwa kwa baadhi ya sehemu za starehe zenye viashiria vya uvunjifu wa amani, hususan maeneo ya Masaki na Oysterbay mkoani Dar es Salaam, pamoja na maeneo mengine yanayohusika ili kudhibiti matishio hayo.

Katambi pia ameagiza kila mgeni anayelala katika nyumba za kulala wageni kuandikishwa kwenye daftari la wageni kwa kutumia kitambulisho cha NIDA.

No comments