HATUTAMFUMBIA MACHO ANAYEPANGA MAANDAMANO HARAMU


Serikali imesema haitamfumbia macho wala kumuonea huruma mtu yeyote anayepanga maandamano haramu yasiyo na kibali katika kipindi hiki, na kwamba tayari Jeshi la Polisi limekamata watu kadhaa na litaanza kuwahoji kuanzia kesho.


Akitoa taarifa ya Serikali baada ya Mbunge wa Dodoma, Pascal Chinyele, kuomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya Kudumu ya 79, akitaka taarifa ya serikali kuhusiana na matishio ya maandamano yaliyopo kwenye mitandao ya kijamii, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema tayari hatua zimeanza kuchukuliwa kukabiliana na matishio hayo.

Waziri Katambi amemuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camillus Wambura, kutoa maelekezo kwa Makamanda wa Polisi wa mikoa na wakuu wa Polisi wa wilaya pamoja na polisi kata kuhakikisha wanaweka mpango madhubuti wa kukabiliana na matishio yote ya uvunjifu wa amani yanayotokea katika maeneo yao.

No comments