Spika wa Bunge Mussa
Zungu, amewataka Watanzania kuendelea kununua bidhaa zinazozalishwa nchini kama
njia ya kuunga mkono viwanda vya ndani na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Akiongoza mamia ya wananchi, viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali katika
matembezi ya hisani ya Jubilei ya Dhahabu ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam (Sabasaba), yaliyofanyika leo Juni 27, 2026, kutoka Shule ya
Polisi hadi Viwanja vya Sabasaba, Zungu amesema ni wakati wa kila Mtanzania
kuonesha uzalendo kwa kuunga mkono bidhaa za ndani.
Aidha, amewataka vijana kuthamini amani na kuepuka kutumika katika vitendo
vinavyoweza kuhatarisha mustakabali wao, familia zao na taifa kwa ujumla.
Akihitimisha matembezi hayo, Zungu amesema yamekuwa mwanzo mzuri wa maadhimisho
ya Jubilei ya Dhahabu ya Sabasaba na jukwaa muhimu la kuhamasisha wananchi
kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa nchini.
Post a Comment