MAMA ASHUHUDIA HISTORIA YA VIZINHA KOMBE LA DUNIA



 Katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Kombe la Dunia 2026 Cape Verde dhidi ya Hispania, golikipa Vozinha aliandika historia kwa kuwa gumzo duniani baada ya kutoruhusu bao lolote na kufanya ‘saves’ za kutosha akiwa na umri wa miaka 40, akicheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.


Kwa bahati mbaya, mama yake Vozinha hakuweza kushuhudia tukio hilo uwanjani kutokana na matatizo ya kupata visa.

Lakini baada ya usiku huo wa kihistoria, changamoto hizo zilitatuliwa na Mama aliweza kusafiri hadi Marekani kumshuhudia mwanae akicheza michuano hiyo.

Hatimaye alipata nafasi ya kumwona mwanawe akiandika historia tena, akiweza kupata clean sheet nyingine na kuisaidia Cape Verde kufuzu hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia.

Mama yake alishangilia kila save kana kwamba timu yake imefunga bao. Ilikuwa ni wakati wa kugusa hisia za wengi.

Baada ya mechi, mama na mwana waliweza kushiriki pamoja furaha ya mafanikio hayo makubwa. Ni tukio lililoijaza fahari si familia ya Vozinha pekee, bali taifa zima la Cape Verde.

Cape Verde ndiyo taifa lenye idadi ndogo zaidi ya watu kuwahi kufuzu hatua ya mtoano katika historia ya Kombe la Dunia la FIFA.

Wakiwa kwenye kundi moja na Hispania, Uruguay na Saudi Arabia, wengi hawakuwapa nafasi yoyote.

Lakini wamewashangaza wote na bado hawajapoteza hata mchezo mmoja.

Sasa wanajiandaa kuvaana na mabingwa watetezi, Argentina katika hatua ya 32 bora ambapo mchezo utapigwa Ijumaa Julai 03 2026.

No comments