NAOMI ADHIHIRISHA MICHEZO NA MAVAZI VINACHANGAMANA

 





Nguli wa tenisi duniani Naomi Osaka ameendelea kuthibitisha kuwa yeye si staa wa mchezo pekee, bali pia katika mitindo baada ya kufika  kwenye mashindano ya Wimbledon akiwa katika muonekano wa kipekee uliovuta kila jicho lililomuona, ‘Japanese inspired Wimbledon look’

Naomi alivaa kimono cha rangi nyeupe iliyobuniwa kulingana na dress code ya Wimbledon, ikiwa na mikono mipana inayopepea na nakshi za kisanii zilizoongeza unadhifu.

Kiunoni aliikamilisha kwa mkanda wa Obi pamoja na obijime zilizofungwa kwa mafundo ya kitamaduni iliyokuwa zaidi ya mitindo kwani ilikuwa na iliwasilisha utamaduni.

Vazi hilo lilibuniwa kwa ushirikiano na mbunifu wa Kijapani Hana Yagi huku Osaka akiunganisha na sleek bun, white wristband na raketi yake ya tenisi, akionesha kuwa unaweza kuheshimu utamaduni wako bila kupoteza moyo wa ushindani, usafi, Fahari na kujenga utofauti.

Walio halisi wanajua…mitindo inapokutana na utamaduni ndipo huzaliwa nyakati zisizosahaulika. Naomi Osaka ameonyesha kuwa wakati mwingine mavazi yanaweza kuzungumza kwa sauti kubwa kuliko maneno.

No comments