JAPAN YAAGA KOMBE LA DUNIA LAKINI WAACHA HISTORIA
Japan imeaga Kombe la Dunia baada ya kufungwa na Brazil, lakini imeondoka ikiwa imeacha somo kubwa kuliko matokeo ya uwanjani.Baada ya filimbi ya mwisho, wakati mashabiki wengi walikuwa wakiondoka kwa huzuni, mashabiki wa Japan walibaki uwanjani wakikusanya na kusafisha taka walizoacha. Hawakufanya hivyo kwa sababu walishinda, wala si kwa ajili ya kamera au kutafuta sifa.
Huu ni utamaduni waliokuzwa nao tangu utotoni—kuheshimu sehemu wanayotumia na kuiacha ikiwa safi kwa wengine. Ni ishara ya nidhamu, uwajibikaji na shukrani.
Matokeo ya soka hupita, lakini maadili hubaki. Ndiyo maana Japan inaendelea kuheshimiwa duniani, si kwa ubora wake wa mpira pekee, bali pia kwa tabia na utamaduni wake wa kipekee.
Michezo ya leo nj Ivory Coast vs Norway (saa 2 usiku), Ufaransa vs Sweden (Saa sita usiku) na Mexico vs Ecuador (Saa kumi alfajiri).
.jpg)

Post a Comment